Q Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.

Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha Makutano, Qchilla amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.

Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo.

Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.

Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia alikuwa aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.

Q Chilla amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani tu na kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.

Kusikiliza au Ku-download mahojiano yote na Qchilla bofya hapa: https://soundcloud.com/makutano-na-fina-mango/makutano-show-mahojiano-na-1
QChilla akiongea katika kipindi cha Makutano Magic FM
Fina Mango akimsikiliza QChilla wakati akijibu moja ya maswali katika kipindi.
Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akiwa na QChilla na mwanae Nuru baada ya kipindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ukipata mafanikio lazima watu wenye choyo na gere wakufuate. Ulikuwa uwe mungalifu.

    ReplyDelete
  2. Sikiliza vizuri bro!! Hapo bongo hakuna mtu yeyote and I mean yeyote mwenye uwezo na kipaji cha kuimba kama wewe, si diamond wala Ali Kiba wana bahati zao tu lakini katika swala la kuimba you are the tops bro na mimi niko nje na nimewasikilizisha wazungu, wanigeria, wahaiti, jamaicans and people from different parts of the world muziki wa kwetu na wote wanakoma na wewe so GET SERIOUS and FOCUS usiwe na mapose wala pretence kama star, just do your thing bro kila mtu will soon be saying what am sayin 2day. Kufanya kosa si kosa kurudia kosa is just foolishnes, make sure you learned from yours.......PEACE

    ReplyDelete
  3. Allah Akbar.. jamaa ndo alivyo sasa??? kweli hujafa hujaumbika

    ReplyDelete
  4. Hawa ndiyo vivuli vya jamii yetu, mambo yao ndiyo haya . . . .
    Nampongeza yeye jwa kujinasua.

    ReplyDelete
  5. Kwa nini unawalaumu watu wengine bila ya wewe mwenyewe kuchukua responsibility?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...