Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha kwenye mkutano wa Chadema Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni akiwa ndani ya gari ya jeshi baada ya kutiwa nguvuni, 
 
  Picha juu alipopiga picha na Viongozi mbalimbali wa Chadema
Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni.
---
Yule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha Monduli ametiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari, ila aliwahi kuwa JKT na akaacha.  Imeelezwa kuwa amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi wa Mererani wanamtambua kama mwanajeshi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. How about his freedom of expression?

    ReplyDelete
  2. How about his freedom of expression?

    Freedom of expression within the context of law!

    Freedom without self-discipline is lunacy!

    ReplyDelete
  3. Anony no1. hes being detained because he has been posing with official Army uniform whist not being one and that is illegal.

    ReplyDelete
  4. Sasa amekamatwa na polisi au na JWTZ? Kwa hiyo ndiyo wanaenda kummaliza huko ndani. Ingekuwa ulaya angetendewa haki.

    ReplyDelete
  5. What if angepiga na mhesimiwa rais?

    ReplyDelete
  6. Huyu ni kibaka tu, active askari wa ngazi hiyo hawezi kuwa na ndevu kama huyu bwana.

    ReplyDelete
  7. Wrong person!

    ReplyDelete
  8. Anon, Rais apige picha na kibaka ili iweje? Na ni ulaya gani ambako vibaka wanapita mitaani wakidai na kupewa haki ya wanajeshi?

    ReplyDelete
  9. Asionewe kabisa kisa kapiga picha na watu wa CHADEMA ana haki ya kupiga picha na mbunge wake kwa sababu mbunge ni kiongozi wa watu wote anaweza kupiga picha na mtu yoyote. Hata hivyo Mhe. Lema hakuvaa sare za chama, alama ya vidole viwili si mali ya CDM ni inshara ya amani duniani kote inatumika. Haya magwanda ya kijeshi si mali ya JWTZ pekee duniani kote yanavaliwa na watu wengi ye si wa kwanza kuyavaa, hasa huwa yanakuja na mitumba kuna mpaka fulana za mabaka mabaka ya jeshi. kama alijitambulisha yeye ni mwanajeshi na si mwanajeshi kuna ushahidi?

    ReplyDelete
  10. Wako wengi jeshi kuweni makini kuna mwanajeshi mmoja alikuwa jwtz ameacha lakini mpaka Leo anatumia kitambulisho cha jeshi kunyanyasa wananchi mmulikeni huyo nae anaitwa Warburg tupelo usisikie kwa kitambulisho hicho hicho cha jeshi kana huyo jamaa

    ReplyDelete
  11. mi hao wanaojiita makamanda tu! Hivi inahitaji uwe na PhD kujua kuwa si halali mtu asiekuwa askari kuvaa sare za askari? au inahitajka PhD kujua kuwa askari ktk guo za kazi haruhusiwi kujihusisha na siasa?
    Wamekaa kama viponzo na pozi zao za picha na huyo kibaka

    ReplyDelete
  12. Nenda kaombe kazi kuwa baunsa wa chadema. Kila kazi ina masharti yake na kwa vile umeyavunja, kwaheri na fika salama.

    ReplyDelete
  13. Hebu nishike jembe nikalime mie......

    ReplyDelete
  14. huku ughaibuni tunajivalia magwanda kwa raha tuu.

    Mbona wenge BCBG hamkuwakamata walivyowaibia wimbo wa pentagoni?

    ReplyDelete
  15. majeshi ya nchi masikini yanaona hata nguo dili, wakati wenzao wanajenga mitambo ya kwenda Mars.

    ReplyDelete
  16. Mwachani mjeshi feki akavune alichopanda lupango!

    ReplyDelete
  17. KWANI KUNA UBAYA GANI KUPIGA PICHA NA HUYU JAMAA?YEYE SIO MUNGU NI BINADAMU KAMA SISI ACHENI UBAGUZI.MDAU CHALTON.

    ReplyDelete
  18. Jamani tuone maoni yenye hoja.....acheni mambo ya chama.....huyo ni kibaka....tapeli....nk.......wacha ashughulikiwe vizuri............ni ughaibuni gani watu wanavaa uniform za jeshi , police ama fire na kulanda landa barabarani...........hata sisi uko ughaibuni tumefika.....sheria inaheshimika kuliko kitu chochote...acheni siasa........

    ReplyDelete
  19. Mbona mnamuonea jamaa kwa ajili ya kuvaa magwanda ya jeshi? Kosa lake mbona aliigharamu serikali chochote, bali muda wa serikali walioupoteza kufuatilia. Mie nilikuwa napinga ili la magwanda ya jeshi toka enzi serikali inawasumbua East Coast na King GK, hata kujadili ili ni kupoteza muda. Mbona Mafisadi na waizi wakubwa wa mali za Taifa inachukua miaka kibao kuchunguza na mpaka leo uchuguzi unaendelea? Na nyie mnaotetea serikali hamlalamiki kuhusu ilo ambalo ndilo linatukwaza ki kweli? Au ndiyo kila kitu afacho Malikia ni Mungu? NAOMBA TUAMKE WATANZANIA.

    ReplyDelete
  20. Wote mnao muunga mkono vichwa vyenu vina matatizo kwenye kufikiria sana.Hivi kila mmoja akiwa ataachwa avae kama mwanajeshi itakuwaje? Na hao watu wanatumia sare za wanajeshi na kufanya uhalifu wakijulikanika kama wanajeshi alafu mnakuja kulalamikia wizi na ujambazi. Tafakari kwanza kabla ya kuzungumza sio unashabikia chama tuu. Ulaya watu wengi wastaarabu hata wakivaa kama hivyo hakuna matukio ya ujammbazi au wizi kwa kutumia sare za jeshi. Nchi itaendelea kwa kutumia akili zenu kikamilifu na si kushabikia upuuzi tuu

    ReplyDelete
  21. yaani huyu jamaa naona kwanza anaenda kuchezea kichapo kabla hawajamwachisha kazi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...