Ankal,
Taswira -video Jijini Dar es salaam ya safari kwa kutumia bajaji toka Kawe, Drive-In, Morocco, Namanga, Salender, Seaview, Red- Cross, Ohio, Garden mpaka Posta.
Mdau Mesiaki
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Asante sana mdau kwa VIDEO yako jambo la kwanza napenda kuwajulisha wadau ni namna gani tunaweza kuona kasoro ndogo ndogo au kubwa kubwa za sheria za nchi na ujenzi wa nchi
ReplyDelete1.unaweza kuona ni hatari ya hali ya juu sana kila anapopita mdau hapo barabarani utaona mtu kasimama anasubiri kuvuka barabara pasipo hata na zebra alama ya kuvukia
2.unaweza kuona ni ya hali ya juu sana huyo muondesha BAJAJI kwa kupita njia ya watembea kwa miguu ili kuokoa kukaa kwenye foleni
3.huo ujenzi wa barabara na muonekano wa mji kuwa ni mchafu kutokana na pembezoni mwa barabara kuonekana michanga au udongo
na badili yake kungependeza zaidi kama wangejengea hizo njia kwa matofali ili zitumieka kwa watembea kwa miguu na baskeli
4.uwekaji mbaya wa matangazo ya biashara yani MABANGO yanawekwa kiholela na kuchafua utanashati wa mji
5.Safari nzima ya mdau mpaka alipofika bila shaka ni zaidi ya KM 5 bila kuona hata gari moja ya polisi wa usalama wa barabarani na raia kwa ujumla
kutokuwepo na magari ya usalama kwa kipande kirefu husababishwa uharifu mkubwa wa maisha ya kibinadamu WIZI, UVUNJAJI SHERIA BARABARANI, USAIDIZI WA HALI NA KISHERIA KWA WATAKAOPATA AJALI,N.K
Mdau wa
dunia iliyopiga hatua.EU
Hizi Bajaj zinasaidia Usafiri lakini kwa upande mwingine ni hatari sana kwa usalama achilia wa waendao kwa miguu bali waliopo ndani ya chombo chenyewe, ni vile Bajaj bodi yake ipo nusu uchi hivi hivyo chombo wacha kuangakuka kabisa kikiyumba basi inakuwa hatari, unaweza kujikuta upo chini ukiwa chaliii au ukafikia tumbo ama utosi aridhini!!!
ReplyDeleteUbahili mwingine jamani?
ReplyDeleteUnakuta mtu unatokea Kawe hadi katikati ya Jiji la Darisalama kwa Bajaji huku mpango ulionao kibindoni ni wa Mamilioni ya Shilingi au kwa uchache Malaki!
Kwa nini usikodi Teksi?