MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Taifa ( UWT), Sophia Simba (aliesimama), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,ameshangazwa na kitendo cha Diwani wa Kata ya Nyandira kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Luanda Zengwe ,kushindwa kuwaondolea wananchi wake kero mbalimbali tangu achanguliwe ikiwemo kushirikiana na Halamshauri ya Wilaya a Mvomero kuwezesha kupatikana kwa kitanda maalumu cha kubeba wagonjwa.
Badala yake amekuwa mstari wa mbele kuwahamisha vijana na wanachama wa chama hicho na pia kuzomea na kuwaletea fujo viongozi wa Serikali ya chama Tawala ( CCM) wanaotembelea kwenye Kata hiyo kwa madhumuni ya kukutana na wananchi ili kupata kero zao mbalimbali na kuzitolea majawabu ya msingi.
Mwenyekiti wa Taifa wa UWT, alishangazwa na hatua hiyo ya kushindwa kutatua kero hizo na badala yake kuondoka eneo la meza kuu Chadema na kwenda kuwahamasisha wafuasi wake wafanye fujo wakati wa mkutano ulioanmdaliwa na UWT kwa wananchi wa Kata ya Nyandira.
Diwani Luanda alipandwa na munkari, baada ya Diwani wa zamani wa CCM wa Kata hiyo , Modesta Lubasije kuwasilisha kero kwa Mwenyekiti wa Taifa wa UWT juu ya ukosefu wa kitanda cha kubeba wagonjwa ‘ Strecha ‘ hasa akina mama wajawazito kwenye Zahanati ya Kijiji cha Nyandira hali inayosababisha kutumia machela za miti.
Kutokana na hoja hiyo, Mwenyekiti wa UWT Taifa na Waziri alimgeukia Diwani waliyekuwa ameketi pembezoni mwa meza kuu na kumtaka wakati ukifika awezekujibu kero za wananchi na wapigakura wake , alitolee majibu huku akimsisitizia kuwa suala hilo si la Waziri bali lipochini ya uwezo wa Diwani kwa kushirikiana na Diwani wa Viti maalumu wa Tarafa ya Mgenta pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.
Hata hivyo kufuatia kuelezwa suala hilo, Diwani huyo alinyanyuka ghafla kutoka meza kuu na kuanza kutoa maneno makali ya kejeri na kumshutumu Waziri Simba kwa kudai swali hilo lililenga kuchafua na hivyo kusababisha kuzuka kwa tafrani za dakika kadhaa na baadaye mkutano kuendelea kama kawaida.
Kutokana na kitendo chake cha kutoa lugha chafu mbele ya Waziri Simba, alimua kunyanyuka na kuindoka meza kuu na kwenda kwa wafuasi wake ambao walijipanga kufanya fujo na kuanza kupiga mayowe na kurushiana vijembe hali iliyowafanya baadhi ya Viongozi wa CCM na UWT chini Katibu wa CCM Wilaya ya Mvomero,Sadakati Kimati kwenda kumdhibiti Diwani huyo wakisaidiwa na Askari Polisi wa eneo hilo.
Waziri Simba akiendelea na mkutano huo, aliwataka wananchi kuona umuhimu wa kuchangua viongozi wenye busara na hekima , kwani kitendo cha utovu wa nidhamu uliooneshwa na Diwani wa Kata hiyo ni kuonesha ni namna gani siasa ya Vyama vya Upinzani zilivyo hapa nchini.
Akizumza kama Mwenyekiti wa Taifa wa UWT, Simba aliwahimiza wana CCM na wananchi wa Kata hiyo kutofanya makosa wakati wa uchaguzi mkuu ujao na badala yake warejeshe uongozi wa CCM katika Kata hiyo.
“ Wananchi wa Nyandira hii ndiyo siasa za wenzetu hawa , baada ya kujionea mwenyewe, ninaahidi panapo majaliwa mwaka 2015 nitatia timu hapa kuendesha kampeni ya nguvu ili Kata hii isiendelee kuwa chini ya watu walevi , ambao hawataki maendeleo ya wananchi “ alisema Simba.
Hata hivyo alisema, maendeleo lazima yaletwe na wananchi kwa kushirikiana na viongozi , hivyo burasa inahitajika pale viongozi wanapofika kwenye eneo kama hilo na wananchi wanayo haki ya kutoa kero zao na kuzipatia majawabu ya msingi.
Kufuatia ombi hilo , Waziri Simba aliahidi kutoa fedha za kununua kitanda maalumu cha kubeba wagonjwa katika Zahanati hiyo ya Kijiji na kuwataka wananchi wenye kupenda amani wampuuze Diwani huyo pamoja na wafuasi wake ambao wao hekima na busara zimewashinda.
Kwa upande wake Diwani Luanda, alidai kuwa , ziara ya Waziri Simba haikuwa ya kiserikali na badala yake ililalia kwenye Chama chake zaidi na yeye kama Diwani wa Chadema wa Kata hiyo alikuwa na wajibu na haki ya kuona wanachama na Chama chake hakichafuliwi.
Zengwe lilianzia hapa ambapo Diwani wa Kata ya Nyandira kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Luanda Zengwe (katikati) aliponyanyuka na kuanza kujibizana na Diwani wa zamani wa CCM wa Kata hiyo ,Modesta Lubasije aliyekuwa akiwasilisha kero mbali mbali kwa Mwenyekiti wa Taifa wa UWT,Mh. Sophia Simba (kushoto).
Katibu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Mvomero, Sadakati Kimati akimdhibiti vilivyo Diwani wa Kata ya Nyandira, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ), Luanda Zengwe, (mwenye skafu), mbele ya Askari Polisi, Sajini Taji aliyefahamika kwa jina la S .E Mndeme kutoka Kituo cha Polisi Mgeta , mara baada ya kutoa maneno ya lugha chafu kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto, Sophia Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Taifa ( hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata hiyo , Januari 19, mwaka huu, Diwani Luanda alikaribishwa akiwa ni mwakilishi wa wananchi kuketi meza kuu.
Diwani wa Kata ya Nyandira kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Luanda Zengwe akiingilia mkutano huo na kuanza kuongea na Wananchi wa Kata hiyo.
Mhh kwa mtaji huu hatufiki mbali watu wanapigana baada ya kusaidia jamii wanavutia itikadi za vyama vyao??? huyu jamaa wa chadema anashindwa kujibu hoja za msingi na anahamasisha watu walete walete vurugu je kwa mtaji huu tutafika wapi?
ReplyDeleteLUANDA ZENGWE,
ReplyDeleteacha MIZENGWE yako kama jina lako lilivyo, sasa ulipogombea Udiwani lifikiri Uongozi ni rahisi?
Mhe. ZENGWE,
ReplyDeleteWaliokupa jina wampatia kwa kuwa utendaji wako na jina lako ni sawasawa,
Jina lako:ZENGWE,
Utendaji :ZENGWE,
Formula ime balance kweli kweli!
Kamwite Godbless Lema na John Mnyika wakusaidie, wewe ulifikiri Uongozi ni lelemama?
ReplyDeleteSasa ziara ya kiserikali mbona wamevalia kijani na huyo diwani magwanda, halafu hiyo mipashano wala haiwasaidii wananchi wa kawaida wao wamelamba posho hapo hapo wanaleta ze comedy.
ReplyDeleteHapa waziri hakutumia busara, huwezi kugeuza mkutano wa serikali kuwa wa kichama. Kibaya zaidi alikuwa akipiga kampeni wakati uchaguzi ulikwisha pita. Diwani hakupaswa kupandisha jazba ila angesubiri wakati wake wa kuongea ufike ndio amkosoe waziri mbele ya wananchi halafu ajibu tuhma.
ReplyDeleteHi habari ina mushkeli , yaani kweli serikali yote ya CCM na madiwani wote wa CCM wameshindwa kutoa kitanda sababu ni diwani mmoja wa CHDEMA?
ReplyDeleteni kazi ya serikali kuhudumia wananchi maana wao ndio wanakusanya kodi mbali mbali halali .... viongozi wa kisiasa kazi yao ni kuisimamia, kuikosoa na kuishauri serikali
ReplyDeleteshida ya tanzania viongozi wengi hasa wa CCM wanawafanya wananchi mazuzu ... wanafanya kama hizo huduma za jamii kwa wananchi ni msaada ... kila kitu ni mtu kachanga, kajitolea, msaada, mkopo etc .... HATUTAFIKA NAMNA HII ... serikali ifanye kazi zake na wanasiasa wafanye kazi zao!
Hivi Diwani wa chama cha upinzani anaweza kweli kuondoa kero za wananchi wake kama serikali kuu aimpi ushirikiano? Waliotoa maoni hapo juu ambao wanamshambulia huyu diwani sioni kama ni sahii. Pia nashangaa ziara za kiserikali mtavaaje nguo za chama mimi nazani bado watz tunashida kidogo hasa ninyi mliopo kwenye chama kinachoongoza kwani mnaona itakuwa vp siku mkinyimwa lidhaa ya kuongoza nchi hii.
ReplyDeleteAnony Fri Jan 25, 08:18:00 pm 2013 Nikulipe kiasi gani?Unaupo mkubwa sana.Asante sana kwa kushare point ya msingi na hao wanawake wa chama tawala wasome na kulifanyia kazi hilo.Ubarikiwe sana.
ReplyDeleteDiwani ana mawazo mazuri.Huyo sijui mwenyekiti alitakiwa akae mezani na Diwani wa sasa.Sio kero za wananchi anaambiwa na diwani aliyeshidwa kufanya kazi, wakati alipewa nafasi na muda wake umekwisha.Sasa diwani wa zamani anafanya kazi wakati sio diwani,Kweli dunia tambara bovu.Pesa za hicho kitanda mwenyekiti kazitoa wapi?Nina mengi ya kusema.
ReplyDelete
ReplyDeletehabari hii imeandikwa na mwana ccm kwani inahukumu wakati hiyo ilikuwa ni kazi ya wasomaji kufanya hivyo. ccm wameshindwa uchaguzi sasa wameamua kuendelea na kampeni chafu, diwani huyu amechaguliwa hivi majuzi tu. ccm wamekuwa madarakani kwa miaka 50 kwanini hawakununua hiyo machela?
Picha ya mwisho inaonyesha wananchi wapo na nani. Angalia walivyokuwa na furaha na kushanglia wanavyomsikiliza huyo Diwani wa Chadema.
ReplyDelete