Ukuta wa eneo la ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal
umeangukia magari zaid ya 19 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo
bajaji tatu,yaliyokuwa yamepaki
eneo ambalo hutumika kupaki wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeeleza
kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa
kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.
Baadhi ya Maofisa kutoka Jeshi la Polisi wakiangalia baadhi ya magari yaliyoathiriwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta mapema leo asubuhi kwenye eneo la kupaki magari,ndani ya kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani.Ukuta huo ulikuwa ukibomolewa na Mkandarasi ikiwa ni hatua za awali wa kituo hicho kuvunjwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi.
Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
Si Magari tu,hata bajaji pia zimeathiriwa vibaya kama uonavyo pichani.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Afande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi.Picha zaidi Bofya JIACHIE BLOG.
Nilifika pale nadhani jamaa wawe na bima au la wana haki ya kumdai mbomoaji alikuwa hajaweka alama ya kuzuia watu kuingia eneo hilo.Uhandisi huu si sawasawa
ReplyDeleteArrggh kama kawaida yetu uzembe kazini hali hii inasikitisha sana mpaka lini jamani.
ReplyDeleteHuyo mkandarasi atakamatwa baada ya muda akishatoa kitu kidogo basi atarudi hapo na tenda ya kujenga ukuta mpya atapewa yeye pia DAMN!
Mungu mkubwa, yaani watu wamejeruhiwa bila poteza maisha.
ReplyDeletetuanze kukagua majengo yote hapo tz,ujenzi wetu hauna viwango vya kutosha na tuendako vifo vingi vitatokea
ReplyDeletenaona mkandarasi hajachukua tahadhari yoyote wakati anafanya kazi yake,atafanyaje kazi huku kuna magari na watu wanapita bila alama za kuwaonya na kuzingatia usalama. ALIPE FIDIA KWA UHARIBIFU ALIO SABABISHA
ReplyDeleteSerikali iangalie jinsi gani ya kulipa magari hayo , maana bila shaka yapo ambayo yamekata 3rd party insurance na hata hivyo hapakuwa na tangazo la PARK AT OWN RISK
ReplyDeletekwanini serikali ilipe? Hiyo ni kati ya mkandarasi na wenye magari.kama kulikuwa na kibao cha no parking.imekula kwa wenye magari.
Deletemdau USA
Wajameni Bongo Tambarale!!!
ReplyDeleteHivi na hizi Bima zetu za Upatu na Karata tatu huku magari yenyewe yakiwa ya Mikopo sijui itakuwaje!
Si ndio tena kurudishana kwenye usafiri wa 'halaiki' wa mabasi ya Ma Toyota DCM wakati watu walikuwa wamejikomboa kwa kuwa na magari?
Tarehe 9 Desemba, 2012 jioni nilikuwa hapo Ubungo Bus Terminal na niliegesha gari langu kumsubiri mgeni wangu. Nilitoka nje ya gari na kusimama karibu ya ukuta huo, kwa kweli nilichoona na kuniogopesha ni kuwa ukuta huo ulikuwa mrefu na nguzo zake za zege zikiwa ndefu zimechoka, hazikuwa zimeshikiliwa sawasawa.Yaelekea lilikuwa ghala fulani likaezuliwa paa lake na kutumika kuwa sehemu ya kuegesha magari, niliona dalili ya ukuta kuanguka hivyo nikasogea pembeni mbali. Kusema kweli tahadhali yangu ya kuanguka kwa ukuta huo niliiona tangu tarehe 9 Desemba, 2012 na si kweli kwamba mkandarasi alianza kubomoa hivi karibuni. Nawapa pole waliofikwa na ajali hiyo na inafaa walipwe wote na Mamlaka za Ubungo Bus terminal.
ReplyDeleteJohn John
Tanzania bwana! Sasa hapo kudaiana utazungushwa mpaka uchoke.
ReplyDeleteSasa Bwana John John ulichukua hatua gani ukiwa mzalendo unaeipenda nchi yako na wananchi wenzako baada ya kuona ukuta uko hatarini hiyo Dec 2012?
ReplyDeleteKila panapoharibika ndio nafasi ya kujifunza lakini kwa sisi Watanzania, jambo likipita ndio limepita. Kwa maoni yangu ningependa sekta nzima ya ujenzi irekebishwe, kuanzia waziri mwenyewe, sheria za ujenzi pia na ufanyikazi katika ujenzi kwa sababu secta hii ya ujenzi ndio inayoongoza duniani katika wingi wa ajali.
ReplyDeleteBahati mbaya tu wadau!
ReplyDeleteWho built the wall? Lazima wajenzi wa huo ukuta wawe accountable na walio approve wajieleze .
ReplyDeleteUzembe huu mpaka lini?
ReplyDeleteKwa kweli hii inaumiza sana, ukute mtu kachukua mkopo benki kanunua gari halina insurance mbona hapo kazi. Na ukweli mkuu wa maingeener alikua anajua akamwambia msaidizi wake mdogo ambaye pia ni mkandarasi aweke red tape. Unajua tena watanzania yule mkandarasi aliyepewa maagizo akaignore akasema atafanya kesho. Kesho ndio ikawa keshokutwa na hatima yake ukuta ukashuka ulivyo. Nani alaumiwe na kufukuzwa kazi? Poleni woote mliopata hilli janga
ReplyDeleteMdau hapo juu
ReplyDelete...Wajameni Bongo Tambarale!!!...
Usafiri wa 'halaiki' utaona makali yake siku inapokuwa kati ya haya:
1.Mvua inaponyesha ukiwa Kituo cha Basi unasubiri usafiri.
2.Ukiwa na haraka kufanya mambo kwenye majukumu yaliyo sehemu mbali na tofauti.
3.Unapokuta hali ya usafiri wa mabasi ni tete abiria wakiwa wanapandia madirishani.
Asalaleee huwezi kukumbuka gari lako lililoangukiwa na ukuta?
KAMA KULIKUWA NA BANGO LA TAHADHARI ACHA WAKOME TU HAO WENYE MAGARI. KWA SABABU SIKU HIZI BAADHI YA WATANZANIA WAMEKUWA NA KIBURI SANA. LA SIVYO KAMA HAKUKUWA NA ONYO LOLOTE HAPO LAZIMA WALIPWE
ReplyDelete