Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo wapili toka kulia akimkabidhi fedha Bi.Asia Kondo ambae ni mjasiriliamali wa kijiji cha Luhembe alipofika katika hafla ya kutoa mikopo kwa wakina mama wajasiriamali wa kijiji hicho iliyotolewa na Vodacom Tanzania,kupitia mradi wake wa “Mwei” unaotoa mikopo isiyokuwa na riba na kurudishwa kwa njia ya M-Pesa,wanaoshuhudia kulia ni Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon na watatu ni Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Mtendaji wa kata ya Luhembe Bw.Richard Kigave.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo katikati akisaini kitabu cha wageni wa kijiji cha Luhembe mara alipofika katika ofisi za kijiji hicho kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wakina mama wajasiriamali wa kijiji hicho iliyotolewa na Vodacom Tanzania,kupitia mradi wake wa “Mwei” unaotoa mikopo isiyokuwa na riba na kurushwa kwa njia ya M-Pesa,wanaoshuhudia kushoto ni Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na kulia ni Meneja wa mfuko huo Grace Lyon.
Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon akiongea na baadhi ya kinamama wajasiriamali wa kijiji cha Luhembe Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro,waliofika katika ofisi za kijiji kwa ajili ya kukopeshwa pesa na Vodacom kupitia mradi wake wa “Mwei” unaotoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wajasiriamali wanawake wadogo na kuzirudisha kwa njia ya M-Pesa zaidi ya wanawake 154 wamenufaika na mkopo huo kijijini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo wapili toka kulia akifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi fedha Bi.Asia Kondo anaeonesha pesa zake ambae ni mjasiriliamali wa kijiji cha Luhembe Mkuu wa Wilaya hiyo alifika katika hafla ya kutoa mikopo kwa wakina mama wajasiriamali wa kijiji hicho iliyotolewa na Vodacom Tanzania,kupitia mradi wake wa “Mwei” unaotoa mikopo isiyokuwa na riba na kurudishwa kwa njia ya M-Pesa,wanaoshuhudia kulia ni Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon na watatu ni Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Mtendaji wa kata ya Luhembe Bw.Richard Kigave.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo wapili toka kulia akifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi fedha Mkuu wa kinamama wajasiriamali wa kijiji cha Luhembe Bi.Mariam Lugoha anaeonesha pesa zake ambae ni mjasiriliamali kijijini hapo, Mkuu wa Wilaya hiyo alifika katika hafla ya kutoa mikopo kwa wakina mama wajasiriamali wa kijiji hicho iliyotolewa na Vodacom Tanzania,kupitia mradi wake wa “Mwei” unaotoa mikopo isiyokuwa na riba na kurudishwa kwa njia ya M-Pesa,wanaoshuhudia kulia ni Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon na watatu ni Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Mtendaji wa kata ya Luhembe Bw.Richard Kigave.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu,akimuongelesha jambo mtoto Husna Hussen mwenye umri wa miezi(7)aliefika na mama yake mzazi Asha Mohamed kulia katika ofisi za kijiji cha Luhembe Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro,kwa ajili ya kukopeshwa pesa na Vodacom kupitia mradi wake wa Mwei unaotoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wajasiriamali wanawake wadogo na kuzirudisha kwa njia ya M-Pesa,zaidi ya wanawake 154 wamenufaika na mkopo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. wanawake hawa tayari wanahela, kwanini hizo hela msiwape wale akinamama walio hoi kule kijijini kwangu?

    ReplyDelete
  2. Unajua kuwa ukitaka kuisaidia familia au jamaa kwa ujumla, njia bora ni kusaidia wakina mama.Sisemi kuwa wanaume ni wajinga, hasha li Lah, lakini saa nyingine huwa kama wamekunywa togwa.

    ReplyDelete
  3. muwapage na ulinzi wasije wakakabwa bure kuwapa hela hadharani. Jifunzeni watabomolewa majumba yao usiku bure kwa mkopo wa 50 alfu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...