Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawaarifu wadau wote kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF na Tanzania Premier League Board (TPL Board) zinapatikana pia kwenye tovuti ya TFF.

Wote wanaopenda kugombea uongozi katika vyombo hivyo wanaarifiwa kuwa wanaweza kupata fomu hizo kwenye tovuti ya TFF (www.tff.or.tz) na wanatakiwa kulipia fomu hizo katika akaunti ya TFF namba 01J1019956700 iliyoko CRDB tawi la Holland House.

Fomu zikiambatanishwa na risiti ya malipo (receipt) au malipo ya benki (deposit slip) zirejeshwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa mkono au kwa barua pepe (email) ambayo ni tfftz@yahoo.com kabla ya saa 10 kamili alasiri ya Januari 18 mwaka huu.

Kwa wagombea wanaorejesha fomu kwa mkono kuna fomu ya orodha (register) ambayo wanatakiwa kusaini wakati wanakabidhi.

Kamati ya Uchaguzi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...