Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kawe Ukwamani, jijini Dar es Salaa, Peter John (wa nne kushoto mwenye suruali) akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi walioripoti shuleni hapo leo asubuhi kwa ajili ya kuanza muhula wa masomo ya Sekondari baada ya kufalu mtihani wa darasa la saba wa 2012 na kuchaguliwa kujiunga na shule hiyo. Wanafunzi wote waliochanguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari Kidacho cha kwanza, na wale wa sekondari waliokuwa mapumzikoni, wametakiwa kuripoti shuleni hii leo kote nchini. Picha na Sufiani Mafoto Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi siku hizi hakuna sare za wanafunzi? Naona wavulana wengine wana suruali nyeusi, wengine suruali za jeans na wengine kaptula za rangi tofauti. Wasichana nao wengine mitandio ya khanga, wengine myeupe, wengine sketi fupi za rangi tofauti na wengine sketi ndefu. Naomba mnijuze au mimi ndiyo nimechelewa sheria zilishabadilika?

    ReplyDelete
  2. EBU SOMA VIZURI NA UELEWE BWANA, HIYO PICHA UIONAYO SI RASMI KWA MAANA YA KWAMBA LEO NI SIKU YAO YA KUKARIBISHWA RASMI SHULENI HAPO IKIWEMO KUPONGEZWA KWA KUPATA NAFASI YA KUJIUNGA NA MASOMO YA SEKONDARI NA KUPEANA TARATIBU NA SHERIA ZA SHULE HUSIKA, NDIO MAANA HATA WANAFUNZI WENYEWE KWA KUTAMBUA HILO HAWAKUONA ULAZIMA WA KUULAMBA UNIFORMS ZAO RASMI ZA SHULE.ANGALIA TU VIZURI.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa pili acha kamba, hakuna uniform kila mtu anapiga kivyake siku hizi. Ila shule za maana bado unform zipo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...