Tamasha kubwa la vipaji kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 litafanyika katika Ukumbi wa Ikondolelo Lodge Hoteli ya Kitalii Kibamba Jumapili hii, ambapo warembo zaidi ya Thelathini wataingia katika kinyang'anyiro hicho na kuonesha vipaji mbalimbali vikiwemo: Kucheza ngoma, Kuimba, pamoja kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.

Katika Tamasha hilo Maalum Mgeni Rasmi atakuwa Muheshimiwa Iddy Azzan Mbunge wa Jimbo la kinondoni. Sambamba na Hayo Mheshimiwa Azzan atazindua tuzo Mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo zengine mbalimbali.

Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000 , Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000. Tamasha litaanza kuanzia saa nane mchana na kuendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...