Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akionyesha kitabu chenye historia ya kabila la Wapimbwe linalotoka Mkoa wa Katavi (kushoto kwa Waziri Mkuu) ni mmoja wa watunzi wa kitabu hicho,Bwana Peter Mgawe mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii.anaye fuatia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi,Bwana Mselemu Abdallah na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Dkt. Rajabu Rutengwe.sherehe hizo zilifanyika katika mkesha wa kukaribisha mwaka mpya mkoani Katavi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimtunuku Tuzo ya Heshima,bibi Teresia Zakaria kutokana na kushiriki shindano la maisha plasi 2012 alishika nafasi ya kwanza na kuweza kutangaza mkoa wa Katavi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimtunuku RPC wa Mkoa wa Katavi,ACP Dhahiri Kidavashari Tuzo ya heshima ya mkoa wa Katavi ya mwaka 2012 kutokana na uhamasishaji wa jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu yaani Polisi Jamii.kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Dkt. Rajabu Rutengwe na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mbunge wa Mpanda,Mh. Saidi Arifi.sherehe hiyo ilifanyika usiku wa mkesha wa kukaribisha mwaka mpya mkoani Katavi.Picha na Chris Mfinanga.
si ukabila unakataliwa jamani mbona nyie bado unaufatilia/kesho na sisi wasukuma tutatoa kitabu chetu.
ReplyDeleteSpot on Anony wa kwanza, katika moja ya hotuba zake, Mwalimu (RIP) alisema ukabila ni upuuzi mtupu, hatutaki ukabila kwani hauna maana yeyote ile, ukabila una maana pale unapotaka KUTAMBIKA tu, sasa vitaby vya makabila siyo tatizo, tatizo ni viongozi wa nchi kuanza kuviigia debe. Bongo kiama.
ReplyDeletekuandika historia au kuwa na maandishi yanayozungumzia kabila lako si ukabila hata kidogo. Lazima ujitambue wapi umetoka na wapi unakwenda. Kumbuka mtu asiyejua mla na desuri zake ni sawa na mtumwa
ReplyDelete