Ankal na Wadau wako,

Naomba mkae mikijua kwamba kuna Mchezo mchafu umeibuka jijini Dar es salaam hususan maeneo ya Jmall, mtaa wa  Samora na Morogoro Road ambapo watu wengi wa mataifa ya nje huja. 

Kuna huyu bwana (alieshika passport ya mzungu nyekundu pichani)  ndio mtaalam mwenyewe.  Mzungu yuo kwa pembeni akishangaa. Wakikukuta huna kibali cha kukaa bongo wanakubeba kwenye Noah yao kisha wanakupeleka wanakojua wao na njiani wanalazimisha utoe pesa ndipo wakuachie.

Tunaomba wanaohusika wamuwinde na kumchukulia hatua maana anachafua jina la nchi na jeshi la uhamiaji kwa ujumla. Inasemekana aliwahi kufanya uhamiaji kabla hajafukuzwa bila shaka kwa utovu wa nidhamu

Mdau DownTown

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mdau uliyetoa hii Mada ninakupa Big Up sana. Yaani, sisi wenyewe tupo hapo Samora Avenue ni vurugu tupu. Kipindi TCAA walipokuwa hapo IPS kulikuwa na msako wa kila mara lakini toka wahame duh limekuwa FREE MARKET. Ni AIBU tupu, wazungu kila siku wanakabwa kwenye Corridor za Samora Avenue na kuibiwa. Sisi wenyewe tumeshawahi kuwakomboa wazungu walikuwa wameshaonyeshwa visu mchana peupe. Uhamiaji/Polisi ni mita chache toka Samora Av. lakini bado USALAMA HAKUNA. Tuliomba JESHI LA POLISI lifanye kazi yake. Tatizo lingine nionalo kwenye jeshi letu la Polisi, ni hawa Askari, Viongozi wa siku hizi, wanavitambi vikubwa (yaani, wamegeuza matumbo yao duty bins) sijui parade na mchakamchaka hakuna tena!! Na hisi hii inawasabisha uwezo wa kifikiri pia unapungua. Mimi hupenda kuwaangalia wanajeshi wa zamani wa ngazi za juu, wengi bado wako wakakamavu na hawana vitambi. Tunaomba Jeshi letu la Polisi wajikosoe ili utendaji kazi uwe wakifanisi. Mji wa Dar si Salama hata kidogo!!!

    ReplyDelete
  2. Hii nchi ni hatari sana sasa mtu kama huyu mwizi na anatumia ujambazi wake kwenye poto la nchi hii na ushahidi huu upo haina haja kutuma timu hapa kumpeleleza tena kwanini asiekwe ndani miaka 5 kwanza

    Ila tatizo tunafuga wizi na mtu asie na hatia nchi hii ndio anakamatwa na kuwekwa ndani

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa namfahamu nahata jana nilimuona makutano ya Morogoro na Libya na huwa anapenda sana kuvizia wageni pale mgahawa uliopo mtaa wa libya. nitawapa jina lake nikikutana na jamaa mmoja ambae anamfahamu na wengi tunajua yupo UHAMIAJI! NItamlengesha kwa manjagu njaa hivi karibuni.

    ReplyDelete
  4. ukiangalia picha yay pili vizuri utaona wahusika wako watano ambao kwenye picha ya kwanza wanaonekana kama watu wenye shughuli zao..so huop ni mtandao maana wanakua kama wanaangalia halia ya hewa/kuzuga ila unaweza kukuta ndi wanacheza mchezo mzima...tafadhali hawa watu wachukuliwe hatua madhubuti maana watatukimbizia wageni...asante mdau kwa kuliona hilo na kuweza kupiga picha hizi.

    ReplyDelete
  5. jamani mnatakiwa kujua kuwa hakuna tena usalama hapa tanzania polisi ndio hao hao wanafanya nao kazi hawezi kuwa pekeyake lazima huyo yuko na mtu mkubwa tuuu ndio maana anajiamini kiasi hicho inamaana kweli akae adharani na afanye kazi ya hatari hivyo polisi wasijue mmmmh tumekwisha.

    ReplyDelete
  6. Rushwa sasa imetosha!

    Huyo mtu anatakiwa akamatwe !

    ReplyDelete
  7. Hawataweza kumkamata. Authorities watasema wanafanya kazi kwa nguvu zao na kwa raha zao hivyo hawataki kupewa presha. Halafu kwani hawamjui? Wanamjua sana? Je wanamlinda? Kama bado yupo mitaani, jibu ni ndio, wanamlinda kwa sababu hakamatwi. Saa tuanzishe saa tuhesabu kama hata authorities watatoa tamko kuhusu huyu jamaa kwenye vyombo vya habari. Utasikia wakisema, hatukupata taarifa wakati taarifa imeshatoka kwenye Michuzi. Mpaka watukanwe au vurugu zitokee ndio wajitokeze kinoma noma tena wakijikakamua ili waonekane wanafanya kazi. Waziri Nchimbi hupo? Wajibisha hao wafanyakazi wako maana wengi wanalala usingizi hawawezi presha za kukabiriana na waalifu, maana wiki jana walitoa tamko kuwa "hawataki kufanya kazi kwa presha" huku watu wakizidi kuibiwa na kuuawa!

    ReplyDelete
  8. Hii ni hali na mazingira hatarishi kwa kasi ya Uwekezaji nchini.

    Ni kuwa tutaikaribisha njaa nchini Tanzania kama Wageni wenye nia ya kuleta Mitaji yao nchini wata ghairi na kutafuta nchi zingine kama Rwanda ambako hakuna ujinga kama huo hapo.

    Kwa Kagame mchezo?

    ReplyDelete
  9. Jambi la ajabu ktk Tanzania yetu, inaweka kwenda kwa nia njema kutio taarifa hiyo, ukifika huko Idara ya Uhamiaji watakudharau kabisa.

    Ndio kwanza unaweza kuambiwa moja ya majibu haya:

    1.Mhusika wa masuala hayo ameenda kunywa chai njoo baadae ndio utamkuta!

    2.Sawa umeshatupatia taarifa tutalishughulikia 'suala lako' sio suala letu au la nchi yetu!.

    3.'Tayari tunayo taarifa hiyo' lakini huku wakiwa bado wamekaa Ofisini wakiendelea na shughuli zingine.

    ReplyDelete
  10. Ohhh njaa mbaya!

    Mnayakoroga mnafukuzwa kazi bado mnaendelea na kazi miferejini?

    ReplyDelete
  11. Si mnaju ya kuwa kila Nchi ina kitovu chake?

    Je mnajua kuwa kitovu cha Marekani ni Wall Steet New York City?

    Je mnajua kuwa kitovu cha Uingereza ni Trafalgar Square-London?

    Na sasa muelewe kuwa Kitovu cha Dar Es Salaam na Tanzania ni Samora Avenue!

    Hilo Genge zima hapo wamekaa kikazi kazi!

    Wengine wanajifanya wanapita njia!

    Wengine ma-Documents mikononi!

    Wengine wanajifanya wanataka kukatisha barabara!

    Ili mradi funika kombe mwanaharamu apite!

    ReplyDelete
  12. Inawezekana Mtandao huo wa Matapeli unapeleka hesabu huko Makao Makuu ya Uhamiaji kwa makusanyo wanayoyafanya!

    Kwa mazingira hayo nani atawakamata?

    Ina maana Samora nzima hakuna walinzi Binafsi wa Maofisi yote yale, hakuna Polisi Patrol?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...