Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Dionece Chamulesile akitoa hotuba ya kuufunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa TPS Saccos uliofanyika mjini Morogoro.
Wajumbe wa Bodi ya TPS Saccos waliomaliza muda wao wakiondoka meza kuu na kuupisha uongozi mpya. Kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dionece Chamulesile, wa katikati ni Dk Juma Malewa na Stanford Ntirundura waliokuwa wajumbe wa bodi hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifurahia kupata viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho.
Baadhi ya viongozi wapya waliochaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Akiba na Kukopa cha Jeshi la Magereza (TPS Saccos) wakiwa mbele ya wajumbe hao (hawapo pichani). Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Joel Bukuku akizungumza na wajumbe hao. Uchaguzi huo umefanyika katika Hoteli ya Edema, mjini Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mkumbuke pia na mazoezi ya viungo ili miili yenu iwe sawa kwa aina ya kazi yenu ya uaskari.

    ReplyDelete
  2. Penye pesa ni vichwa vya wanaume tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...