Mdau Said Yakub ana urefu wa futi 6 na inchi 2. Lakini alionekana si lolote alipokutana na jamaa huyu toka Pakistan mwenye urefu wa futi nane mjini Dubai. Yeye anajipatia riziki kwa urefu wake maana ukitaka kupiga naye picha lazima zikutoke dola 3 za kimarekani. Na jinsi inavyoonekana huwa halali njaa....
Home
Unlabelled
maisha ni safari ndefu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
du! Saidi unaonekana kama upo na dad anakupeleka kindergarten.....
ReplyDeleteAmetambua kipaji chake na kukuweka penye soko la uhakika na kukitumia ipasavyo. Wewe Je?
ReplyDeleteMimi nasubiri kuchakachua ofisini kwangu kama wafanyavyo viongozi na watanzanie wengi hapa Tanzania. Hatutumii vipaji tunasubiri kuiba, tumekuwa taifa la wezi, waongo, wavivu, n.k.
ReplyDeleteTumekumisi Yakub.
ReplyDeleteMdau Kabo.
Kimfaacho mtu chake.
ReplyDeleteMdau Saidi Yakubu yeye Mpakistan amekuzidi urefu lakini wewe umemzidi kwenye unene!
ReplyDeleteHivyo mmefunikana wenyewe kwa weneywe ningekuwa Refa ningegawa Pointi!
Ama kweli Sheikh wa Pakistan mambo hayo unafanyia huko Dubai ukiwa kwenu Sheria ni kali kwanza hiyo Kofia hutaruhusiwa kuvaa, utatakiwa uave Kibandiko ama Kilemba na suruali utavaa lakini utatakiwa uvae na Nusu Kanzu!
ReplyDeletePia suala la kunyoa ndevu unafanyia majuu ukiwa Pakistan huruhusiwi kwenda kwa kinyozi wa ndevu!
Ama kweli Mdau wa Pakistan hapo Dubai ni kama upo Ulaya vile?
Haya wenye Vitambi Bongo na ninyi mfanye safari za Dubai mkakusanye DOLA zenu, hamjui ya kuwa kitambi kwa wenzetu ni miujiza?
ReplyDeleteMdau wa 5 anony wa Wed Feb 27, 08:51:00 pm 2013
ReplyDelete...Kwa Tanzania yetu Bongo Tambarale mtu kuwa mwizi Kazini kwake anaonekana ndiye mweye akili ya maisha!
Mtu akiwa Fisadi anaonekana Genius mbele za watu!