Mdau Said Yakub  ana urefu wa futi 6 na inchi 2. Lakini alionekana si lolote alipokutana na jamaa huyu toka Pakistan mwenye urefu wa futi nane mjini Dubai. Yeye anajipatia riziki kwa urefu wake maana ukitaka kupiga naye picha lazima zikutoke dola 3 za kimarekani. Na jinsi inavyoonekana huwa halali njaa....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. du! Saidi unaonekana kama upo na dad anakupeleka kindergarten.....

    ReplyDelete
  2. Ametambua kipaji chake na kukuweka penye soko la uhakika na kukitumia ipasavyo. Wewe Je?

    ReplyDelete
  3. Mimi nasubiri kuchakachua ofisini kwangu kama wafanyavyo viongozi na watanzanie wengi hapa Tanzania. Hatutumii vipaji tunasubiri kuiba, tumekuwa taifa la wezi, waongo, wavivu, n.k.

    ReplyDelete
  4. Tumekumisi Yakub.
    Mdau Kabo.

    ReplyDelete
  5. Kimfaacho mtu chake.

    ReplyDelete
  6. Mdau Saidi Yakubu yeye Mpakistan amekuzidi urefu lakini wewe umemzidi kwenye unene!

    Hivyo mmefunikana wenyewe kwa weneywe ningekuwa Refa ningegawa Pointi!

    ReplyDelete
  7. Ama kweli Sheikh wa Pakistan mambo hayo unafanyia huko Dubai ukiwa kwenu Sheria ni kali kwanza hiyo Kofia hutaruhusiwa kuvaa, utatakiwa uave Kibandiko ama Kilemba na suruali utavaa lakini utatakiwa uvae na Nusu Kanzu!

    Pia suala la kunyoa ndevu unafanyia majuu ukiwa Pakistan huruhusiwi kwenda kwa kinyozi wa ndevu!

    Ama kweli Mdau wa Pakistan hapo Dubai ni kama upo Ulaya vile?

    ReplyDelete
  8. Haya wenye Vitambi Bongo na ninyi mfanye safari za Dubai mkakusanye DOLA zenu, hamjui ya kuwa kitambi kwa wenzetu ni miujiza?

    ReplyDelete
  9. Mdau wa 5 anony wa Wed Feb 27, 08:51:00 pm 2013

    ...Kwa Tanzania yetu Bongo Tambarale mtu kuwa mwizi Kazini kwake anaonekana ndiye mweye akili ya maisha!

    Mtu akiwa Fisadi anaonekana Genius mbele za watu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...