Taarifa ya
mkutano wa wanachama wa chama cha mapinduzi wa maeneo ya District of Colombia,
Maryland na Virginia ( DMV)
Wanachama wote wa CCM tunaombwa kuhudhuria mkutano wa
wanachama wote ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuimarisha tawi letu.
Tafadhali
usikose kuhudhuria ili sauti yako isikike na ushiriki kikamilifu kukijenga
chama chetu na kuleta maendeleo ya nchi yetu.
MAHALI: 3621
Campus Drive Park , MD 20740
SIKU: Jumapili, February 24,
2013
SAA: 5.00 p.m
AJENDA
1.
Taarifa fupi ya Tawi
2.
Mikakati juu ya
uimarishaji wa tawi letu
3.
Mjadala wa uchaguzi wa
viongozi wa tawi
4.
Mengineyo
Tafadhali tujitokeze kwa wingi kama ilivyo desturi yetu kina
baba tunaomba msaada wa maji na soda na kina mama kupika chakula.
Asanteni
Imetolewa na ofisi ya katibu
wa Tawi la ccm DMV
Yacob kinyemi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...