 |
Meli ya kivita
ya kupambana na uharamia aina ya Anti Submarine iitwayo Marshal Shaposhnikov’, ilipokuwa
ikiingia na kasha baadae kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara
fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania
na Urusi. Wakati nchi ya
Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia, jumuiya ya kimataifa ilikubaliana
kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu. Lakini hadi sasa, wakati nchi
nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika mapambano hayo, ni nchi za Russia,
India na China pekee zinazosindikiza meli zao za biashara na nyinginezo ili
kuzilinda na uharamia. Meli hiyo imewasili
siku ya Jumamosi na inategemea kuondoka kesho, Jumatano.
|
 |
Balozi wa Urusi hapa
nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akiambatana
na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear Admiral Vdovenko |
 |
Kwa pamoja, Balozi
Rannikh na wanajeshi wa Kirusi waliimba wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.
|
 |
Balozi Rannikh akiwapongeza
wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania na kuwakaribisha nchi pia. |
 |
Baada ya salamu hizo,
Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo iliyoandaliwa na wanajeshi
katika meli. |
 |
Balozi wa Urusi hapa
nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu kutoka kwa kiongozi
mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati alipotembelea meli hiyo bandarini. |
Wanajeshi wa Kirusi
wakionesha umahili wao wa ukakamavu
Warusi hawa hakuna cha keki na mvinyo, hiyo ni vodka kavukavu mchana mchana, watu na tamaduni zao.
ReplyDeleteMrusi huyu,hakuna cha mvinyo hapa,jamaa anapata vodka kavukavu mchana mchana, dumisha tamaduni rafiki.
ReplyDeleteHehehehe Wadau hapo juu,
ReplyDeleteHiyo Keki ni zuga zuga tu kama chachandu tu msije Watanzania mkaanza kulalamika ohhh Warusi wamekuja Kijeshi Tanzania wanalewa tu,
Hawa Warusi si wanatujua Watanzania kwa lawama?
Mambo hapo ni mpango mzima maji ya betriii!!!
hawajama wakofiti mbaya, hakunamwenyemimba hapo... embu uje ucheki wanajeshi wetu kati ya kumi watatu wana mimba. lol
ReplyDeleteMimba (Kitambi)