Naibu Spika na ujumbe wake wakiwa na wenyeji wao katika ukumbi wa Bunge la Majlis Shura nchini Oman.
Katibu wa Bunge la Majlis Shura Sheikh Al Al Mahrooqi (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Spika kuhusu historia ya nchi hiyo.Naibu Spika yuko nchini Oman kwa ziara ya kibunge.
Naibu Spika Mhe.Job Ndugai akiwasilisha ujumbe maalum wa Bunge la Tanzania kwa Spika wa Bunge la Oman lijulikanalo kama Majlis Shura.Naibu Spika na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge wako Muacat Oman kuanzisha mahusiano maalum ya kibunge baina ya nchi hizo mbili. Pichani kulia ni viongozi kadhaa wa Majlis Shura na kushoto ni ujumbe wa Tanzania uliomshirikisha pia Kaimu Balozi Nd.Abdallah Kilima(kwanza Kushoto).
Naibu Spika Job Ndugai akimkabidhi mwenyeji wake ambae ni Spika wa Bunge la Majlis Shura, Sheikh Khaled bin Nasser Al Mawwali zawadi maalum ya jengo la Bunge la Tanzania
Mh Ndugai tafadhali chonde chonde hio picha nakuomba kwa unyenyekevu usiitoe tena kwenye ziara zako maana unatuabisha watanzania. Hio picha kuprint na frame yako haizidi dola 10, si bora ingekuwa picha ya kuchorwa kwa mkono, au kuchongwa kwenye mbao au hata kufinyangwa na hivyo kuwakilisha utanzania wetu??
ReplyDeleteChe
Mavazi ya waarabu yanapendeza sana kuliko suti zetu hizi za Magharibi.Tunahitaji VAZI la taifa siyo siri
ReplyDeleteDavid V
Kama Mwanahistoria, napenda kuwafahamisha wadau kuwa Oman haina Bunge lenye sauti ya demokrasia kama nchi nyingine, ila bunge lao bado linatawaliwa na Sultani wao na yeye pekee ndie anayetoa ruhusa kuwa nani awe mmbunge na nini kisemwe katika "bunge". Kwa kifupi, Oman, kama nchi nyinginezo za kitajiri za Uarabuni, haiwapi haki ya wananchi wao kujitawala kidemokrasia.
ReplyDeleteSasa jamani hayo MAJAMBIA kiunoni ya nini?
ReplyDeleteMakomredi wako wapi maana hudanganya watu Zanzibar kuwa itaungana na Oman ikiwa CUF inataingia Ikulu.
ReplyDeleteHii picha mbona nzuri tu.Jengo la Bunge letu ni kitu cha kujivunia.Bravo Ndugai! Tuwakilishe vyema!
ReplyDeleteWe anon 2.31 unajua maana ya culture?
ReplyDeleteMajlis Shura wanachaguliwa na watu kuwawakilisha watu na wanachapa kazi yao inabuotakiwa
ReplyDeleteNdugu ulieongea kuhusau democrasia ya majlis shura la oman huelewi kitu bora sona zaidi ujifunze maendeleo ya oman na democrasia yake. Kukaa gizani mda mrefu mambo yanakupiga chenga, bora kaa kimya kulikoni kuandika kitu hukielewi.
ReplyDeleteMdau wa nne juu anony wa Sun Feb 24, 02:31:00 pm 2013
ReplyDelete...MAJAMBIA viunoni, ni ya kukabiliana na Maandui na sio kuchinjana wenyewe kwa wenyewe (Busere sere-Geita) kama wanavyofanya hawa Wanaharakati wetu Tanzania!
Hawa watu Wauaji Zanzibar ni wa kuwafikishia Mashitaka huko Bunge la Majlis la Oman.
ReplyDeleteNadhani kule watasalimu amri!
zawadi ya picha ilikuwa inatosha sana. majambia ni mavazi ya utamaduni kwa waarabu . urafiki baina ya tanzania na oman unaleta faida kwa wananchi wa nchi mbili hizi .
ReplyDeletewaomani wanaweza kupata business partners kutoka nchi nyingine bila tabu , lakini kwa sababu ya uhusiano mrefu baina yetu . ni busara ku invest huu urafiki uongeze faidaya uchumi.