Naibu Spika na ujumbe wake wakiwa na wenyeji wao katika ukumbi wa Bunge la Majlis Shura nchini Oman.
 Katibu wa Bunge la Majlis Shura Sheikh Al Al Mahrooqi (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Spika kuhusu historia ya nchi hiyo.Naibu Spika yuko nchini Oman kwa ziara ya kibunge.
 Naibu Spika Mhe.Job Ndugai akiwasilisha ujumbe maalum wa Bunge la Tanzania kwa Spika wa Bunge la Oman lijulikanalo kama Majlis Shura.Naibu Spika na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge wako Muacat Oman kuanzisha mahusiano maalum ya kibunge baina ya nchi hizo mbili. Pichani kulia ni viongozi kadhaa wa Majlis Shura na kushoto ni ujumbe wa Tanzania uliomshirikisha pia  Kaimu Balozi Nd.Abdallah Kilima(kwanza Kushoto).
Naibu Spika Job Ndugai akimkabidhi mwenyeji wake ambae ni Spika wa Bunge la Majlis Shura, Sheikh Khaled bin Nasser Al Mawwali zawadi maalum ya jengo la Bunge la Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mh Ndugai tafadhali chonde chonde hio picha nakuomba kwa unyenyekevu usiitoe tena kwenye ziara zako maana unatuabisha watanzania. Hio picha kuprint na frame yako haizidi dola 10, si bora ingekuwa picha ya kuchorwa kwa mkono, au kuchongwa kwenye mbao au hata kufinyangwa na hivyo kuwakilisha utanzania wetu??

    Che

    ReplyDelete
  2. Mavazi ya waarabu yanapendeza sana kuliko suti zetu hizi za Magharibi.Tunahitaji VAZI la taifa siyo siri

    David V

    ReplyDelete
  3. Kama Mwanahistoria, napenda kuwafahamisha wadau kuwa Oman haina Bunge lenye sauti ya demokrasia kama nchi nyingine, ila bunge lao bado linatawaliwa na Sultani wao na yeye pekee ndie anayetoa ruhusa kuwa nani awe mmbunge na nini kisemwe katika "bunge". Kwa kifupi, Oman, kama nchi nyinginezo za kitajiri za Uarabuni, haiwapi haki ya wananchi wao kujitawala kidemokrasia.

    ReplyDelete
  4. Sasa jamani hayo MAJAMBIA kiunoni ya nini?

    ReplyDelete
  5. Makomredi wako wapi maana hudanganya watu Zanzibar kuwa itaungana na Oman ikiwa CUF inataingia Ikulu.

    ReplyDelete
  6. Hii picha mbona nzuri tu.Jengo la Bunge letu ni kitu cha kujivunia.Bravo Ndugai! Tuwakilishe vyema!

    ReplyDelete
  7. We anon 2.31 unajua maana ya culture?

    ReplyDelete
  8. Majlis Shura wanachaguliwa na watu kuwawakilisha watu na wanachapa kazi yao inabuotakiwa

    ReplyDelete
  9. Ndugu ulieongea kuhusau democrasia ya majlis shura la oman huelewi kitu bora sona zaidi ujifunze maendeleo ya oman na democrasia yake. Kukaa gizani mda mrefu mambo yanakupiga chenga, bora kaa kimya kulikoni kuandika kitu hukielewi.

    ReplyDelete
  10. Mdau wa nne juu anony wa Sun Feb 24, 02:31:00 pm 2013

    ...MAJAMBIA viunoni, ni ya kukabiliana na Maandui na sio kuchinjana wenyewe kwa wenyewe (Busere sere-Geita) kama wanavyofanya hawa Wanaharakati wetu Tanzania!

    ReplyDelete
  11. Hawa watu Wauaji Zanzibar ni wa kuwafikishia Mashitaka huko Bunge la Majlis la Oman.

    Nadhani kule watasalimu amri!

    ReplyDelete
  12. zawadi ya picha ilikuwa inatosha sana. majambia ni mavazi ya utamaduni kwa waarabu . urafiki baina ya tanzania na oman unaleta faida kwa wananchi wa nchi mbili hizi .
    waomani wanaweza kupata business partners kutoka nchi nyingine bila tabu , lakini kwa sababu ya uhusiano mrefu baina yetu . ni busara ku invest huu urafiki uongeze faidaya uchumi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...