Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipeana mkono na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulembe wakati ujumbe kutoka shirika hilo ulipofika ofisini kwake kuandikisha viongozi wa Serikali katika Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF mjini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akijaza fomu ya uanachama wa Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka saini ya dole gumba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ofisini Kwake Vuga mjini Zanzibar baada ya kujiunga na NSSF. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Dodoma, Mariam Ahmed, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu na Ofisa Uendeshaji NSSF, Ally Mkulemba.
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akimkaribisha ofisini kwake Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed alipofika kwa ajili ya Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akifafanua jambo kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo. Kulia ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akiweka saini ya dole gumba.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.
Sawa NSSF kutua Zanzibar ndio sehemu ya Muungano.
ReplyDeleteJe ni vipi hatma ya ZSSF (Zanzibar National Social Security Fund) huko Visiwani?
Je nayo ZSSF kwa nini isije hadi Bara kujitanua?
Hii ndio kasi ya Muungano inayotakiwa:
ReplyDeleteNi muhimu Watanzania wote Bara na Visiwani wakatambua ya kuwa ''Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'' ni nchi hai, haijazirai wala haijakwenda Likizo kama wengi wanavyofikiri.
Muungano una nguvu, ndio kama hivi sasa tunaona upanukaji wa Huduma za Mifuko kufanya shughuli zake huku Mifuko ikiwa huru kujitandaza wigo wake nchini Bara na Visiwani.
Inatakiwa Mifuko yote ikiwemo ZSSF (Zanzibar Social Security Fund) iwafikie wananchi wote Bara na Visiwani na vivyo hivyo Mifuko mingine kama hivi (NSSF) iingie hadi Visiwani !
Baada ya majukumu mazito Mhe. Raisi wa Zanzibar Dr. Shein anasubiriwa kwa hamu katika mchakato wa Uraisi Muungano!
ReplyDeleteTunayo matumaini makubwa na Uongozi wako!!!
NSSF ndani ya Zanzibar,
ReplyDeleteWapinga Mapinduzi na Wapinga Muungano tunawasubiri hewani, kwa maoni yetu!
Khabari ndiyo hiyo!
Unaposikia mara zote vitu kama,
ReplyDelete-Ushirikiano wa nchi kadhaa,
-Umoja wa nchi kadhaa,
-Muungano wa nchi kadhaa,
-Shirikisho la nchi kadhaa,
-Jumuiya ya nchi kadhaa,
Sio kitu cha kukebehi, na wala (isichukuliwe ni kama kichwa cha mwendawazimu), pia tuelewe ya kuwa maamuzi ya kufikia mojawapo ya hatua hizo hapo juu mara nyingi hufanywa na watu wenye akili nzuri na mawazo yaliyo pevuka.
Mfano katika eneo letu la Afrika ya Mashariki nchi kama Kenya isingehitaji lolote kwenye Ushirikiano wa nchi ikiwemo nchi masikini kama Burundi ndani ya hiyo EAC!
Isipokuwa kutokana na mahitaji ya Ukuzaji na maendeleo, hakuna nchi inayotosheka huhitaji zaidi MUUNGANO mara zote!
Kwa taarifa zaidi hata kama Ujerumani yenye uchumi ulioimarika zaidi katika Umoja wa Ulaya na angalau ktk nchi za Dunia, ingelikuwa Kijiografia imo ktk eneo letu la Afrika ya Mashariki bado ingelihitaji kujiunga na Muungano huo pia!
Jogoo wa Muungano anazidi kunawiri na kukung'uta mbawa zake Visiwani!
ReplyDeleteMsinze kudai NSSF kuingia Visiwani nayo ni kero ya Muungano?
Mmekuwa mabubu kwa muda Wapinga Muungano!
ReplyDeleteAu midomo imewekwa gundi?
Vidole navyo je?, kutuma Maoni hata key boards za Computer zimekuwa za moto?
Wapinga Mapinduzi na Muungano kilichobaki ni kuhamia Baharini mkaishi na samaki!
ReplyDeleteVitambulisho vya Taifa, mnaleta kigugumizi!
Kila kitu mizozo tu!
Ahhh mbona hambebeki?