Uongozi wa mtandao huu
umesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa blogs, kuwa
wakiiba kazi za watu katika blogs mbalimbali yaani ‘Kukopi na Kupaste’ kutoka
katika blog Fulani na kuweka katika Blogs zao bila kujali haki miliki ya kazi
ya mtu, wala kumpa haki yule aliyechukuliwa kazi yake kwa kuandika mahala
ulipochukua kazi hiyo.
Kama inavyojulikana
utafutaji wa habari si lelemama na ikumbukwe ili kupata habari iliyo bora na
itakayowafurahisha wasomaji wako, kwenda na wakati ni lazima uihangaikie na
katika kuihangaikia kuna gharama kibao zinazotumika, ikiwa ni pamoja na
usafiri, pesa, na hata mafuta ya gari kutoka mahala Fulani kwenda sehemu
nyingine, gharama za simu na hata kuwalipa wale unaowatuma ili kukufanyia kazi
hiyo.
Kama umeweza kufanya
mambo yote hayo kwa gharama unazozijua wewe uliyeweka stori, ama picha katika
Blog yako, halafu watu wenye Blog Fulani wasio na uwezo wa kufanya kazi na
kuchukua kazi yako kana kwamba ameokota tu jalalani na anaweka kwake ili
wasomaji wake wasome, bila kuwajulisha kuwa kazi hiyo iliyomvutia imefanywa na
mtandao Fulani kwa kweli inaumiza, inaudhi na inarudisha nyuma malengo hasa ya
kuwa na mitandao hii, wote tutajaonekana wapuuzi.
Mtandao huu
umewavumilia watu hawa kiasi cha kutosha lakini sasa imezidi kukithiri, kwani
jamaa hawa wapo katika ukurasa wako kukusubiri kuona tu ulichoweka kwa wakati
huo, ili wao wakopi na kupaste kwao, halafu tayari wamemaliza wala hawataki
kujihangaisha kufanya kazi ili kuboresha mitandao yao na kuwavutia wasomaji
wao.
‘Unapoamua kutangaza
vita ujue tayari umeshajipanga kukabiliana na kila litakalotokea mbele yako, na
pia umejipanga katika kutoka upinzani wa kweli ili watu waone na wakutambue,
lakini sio kwa staili hii ya kuomba mtangaziwe blog zenu kupitia kwa wale
walioanza mapema halafu kumbe kazi yenyewe ni kuchukua kazi za watu tu na si
kufanya kazi’ yaani kukopi na kupaste,
Kuna msanii mmoja
alichoshwa na wenzake wanaotamani kuingia kwenye gemu, lakini wanashindwa
kuumiza vichwa kubuni ili kuweza kupata radha tofauti, na kuamua kuwafikishia
ujumbe kwa kuwaimba kuwa ‘Si lazima wote tuimbe kuna michezo mingi hata kucheza
bao kama huwezi kuimba, ikiwa kila wimbo unaotoka mpya umekopiwa, kama si
mashahiri, basi ni Beat,
Na hata katika
mablogger si lazima wote tuwe na Mablogger, kama huwezi kuumiza kichwa utoke
vipi, basi kaa pembeni waachie wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, kukopi na
kupaste hadi mitandao yote inakuwa sawa nini maana ya habari za haraka
mtandaoni?,
Huoni kuwa mnawachosha
wasomaji wenu, kwa kosoma habari na picha zinazofafa kwa wakati mmoja na katika
mitandao yote?,
Tena msomaji wako wakiwa
ni waelewa hawawezi kusoma tena mtandao wako kwani habari kama hiyo hiyo walikwishaiona
katika mtandao Fulani muda mchache uliopita na dakika chache baadaye wanaikuta
vile vile walivyoisoma kwingine ikiwa katika ukurasa wako, mara moja mara mbili
msomaji huyo si umempoteza?’’.
Mablogger acheni uvivu
na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu, na kama ukifanya hivyo basi jitahidi
kumpa credit yule uliyemchukulia kazi yake.
VITU muhimu vy kuwa
navyo ili kufanikisha kazi yako ya Blog, ni Laptop ‘Kompyuta mpakato’, ama Desk
Top, Modem ‘Internet Wireless’, Kamera hata ndogo tu ya mkononi, na pia ujue
maana ya kuanzisha hiyoBlog yako na malengo yako kwa jamii, kwani sidhani kama
unaweza kuanzisha blog ili uwe ukisoma mwenyewe na naniliu wako tu.
Na kuwa na kamera si
bora tu kuwa kamera pia ujue kuitumia ipasavyo ili kunasa picha nzuri uitakayo
na itakayofikisha ujumbe kwa wasomaji wako hata kwa kuiangalia tu, kwa kile
ulichokusudia kuwaarifu wasomaji wako.
Baadhi ya Blogs zenye
tabia ya kukopi na kupaste orodha yake tayari tunayo na baada ya tangazo hili, zikiendelea
tutaziweka hewani ili wasomaji wajue ni Blog ipi ya kweli na ipi ni mamluki.
Ni jambo la muhimu sana umelieleza Bwana Michuzi. Ni vyema kutafuta habari zako kama Blogger. Utashangaa na hili Onyo wanalikopi jinsi lilivyo na kuliweka katika Blogs zao pia.
ReplyDeleteGregory.
Umenena mwanawane..kwa kifupi blogs nyingi za bongo ubunifu ni zero..wengi wanachukua news na pc kutoka kwa michuzi..kama kazi hawawezi c waache??Habari michuzi akiweka subiri dkk tano tu blog zote zitatundika hiyo hiyo habari..kuna dada chem kuna cku aliweka hio hio mada kuwa blog nyingi za wabongo ni kucopy na kupaste kwa kwenda mbele...Jamani fanyeni ubunifu kidogo mnatumia nondo hadi kwenye news teehteeh.
ReplyDeleteYou have said it all. Ila mifano ingetusaidia kuwajua wavivu hao
ReplyDeleteWengi tumeliona hilo, ushauri kwa picha za blog uziwekee signature yako mfano michuzi etc, nimeliona hili kwa kaka Arnold Kayanda, mara nyingi yeye haibiwi picha zake.
ReplyDeleteMICHUZI AFADHALI UMESEMA KWA SA BABU WATU WENGI HAWAPENDI KUSHUGHULIKA NA KUHANGAIKA, WANAPENDA EASY JOBS WAKAE TU NA KUTUMIA JASHO LA WENZAO KUJIPATIA UMAARUFU. UMEANZA MBALI NA UNSTAHILI KUFIKA HAPO ULIPO, WENGINE WANAFIKIRI WANAWEZA PANDA UNGO KUFIKA HARAKA LOL WELDONE YOU
ReplyDeleteWapo wanao copy mpaka matangazo ya biashara (banners) wakati hawana mikataba na makampuni yanayotajwa kwenye hayo mabango.
ReplyDeleteJamani anayelalamika ni www.sufianimafoto.blogspot.com kupitia kwenye blog ya jamii.Ankal yeye 'hanaga' noma, wacopy wasicopy blog ya jamii itaendelea kutesa.
ReplyDeleteIla Sufiani ulichokisema ni kweli,nilishaona na rafiki yangu Mjengwablog analalamikia kitu kama hiki.
David V
tena memba wa jamii forums ni wezi wakubwa kutwa wapo humu kwa ankali michu wananyofoa picha na kwenda kubandika kule kwao, halafu hawasemi wametoa wapi yani wanaboa sana, kazi kujidai ati huwa hawaingii humu kwa michuzi lakini ndo wezi namba moja, nyie mnaojiita magreat thinker mkija kunyofoa picha na habari huku hasa wewe ctu na wenzako muwe mnasema mmetoa kwa michuzi blog, hapo ndo tutaona ugreat thinker na sio udokozi thinker. na sio kujifanya kuwa nyie ndo sorce ya kila kitu wakati ukweli unajulikana.
ReplyDeleteSUBIRI SASA SI UMEANZISHA VIJIMAMBO NA CHEKA UNENEPE...BASI SOON WAJASIRIAMALI NAO WATAANZA KUCOPY NA KUPASTE VIJIMAMBO NA CHEKA UNENEPE...BONGO BANAA WEE ACHA TU KWELI NI DASLAMU!!!
ReplyDeleteMDAU WA KWA MAMA(QUEEN).
Kaka michuzi that is a crime to steal some material .weka majina hapa tuache kwenda Huko .yaani wabongo hatuna ethics .We need to respect people job duh nomaaa
ReplyDeleteTake them to court .jamii forum
ReplyDeletemimi ni mpenzi wa michuzi,miladayo,shamim,uturn mange,miss jestina,nuru the ligth.mjengwa.sijaona saaana ila wanaweza wakawa wanafanya siku moja moja.ila hao wengine wote walio bakia wanakopi na kupesti kwenu.kama nitakua nimekosea mnisamehe.
ReplyDeleteMjomba Michuzi,
ReplyDeleteHaiwezekani majasho yanayo churuzika migongoni mwenu yaende bure bure!
Nafiriki itawalazimu muingie gharama angalau kidogo tu mfanye vitu hivi:
1.Kusajili kazi zako kwa Patent rights , haki miliki.
2.Ktk margin za Habari na Picha zako tumia ujuzi wa Graphics ku block picha na habari zako ili ujikinge na wizi!
Blogs za kibongo ni sawasawa tu na bongo fleva.....kukopi kazi za watu na kuziita zao kisha mtu analilia haki ya kazi yake hailindwi.
ReplyDeletePoleni,ila yote haya ni matokeo ya "Ujamaa" si tulifundishwa tushirikiane.
ReplyDeleteSasa mbona mna hubiri ubinafsi tena.
Ila kwa mtazamo wa aliyelalamika ni kama blog zote lazima ziwe za habari kwa picha? Hivi ni sawa?
Staharisha umesikia ???
ReplyDeleteHili nalo neno ukiingia blog zote utakuta alichopost Michuzi nao wamepost sio Starlisha peke yake ukiingia blog zote za wabongo wanachukua kazi za kaka Michuzi na tena hao wezi wenyewe ktk mablog yao ndiyo wanajitamba utafikiria wametolea jasho hiyo habari au kutafuta hizo pic.
ReplyDeleteMimi naona kama mtu amecopy habari kutoka sehemu furani naona ni njia mojawapo ule ujumbe kusambaa na kumfanya yule mtu wa kwanza kujidai kuwa kazi ameifanya ni nzuri mpaka watu wanaicopy.Mfumo wa kucopy hauwezi kufutika mfano hata wewe hapo ulipo katika CD zako pale nyumbani au Flash ukosi kuwa na nyimbo uliyocopy kutoka mwanamusic hapa dunia mbona ujaenda kukunua orginal copy ili unyanyue kazi ya msanii yule
ReplyDelete