Uongozi wa mtandao huu umesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa blogs, kuwa wakiiba kazi za watu katika blogs mbalimbali yaani ‘Kukopi na Kupaste’ kutoka katika blog Fulani na kuweka katika Blogs zao bila kujali haki miliki ya kazi ya mtu, wala kumpa haki yule aliyechukuliwa kazi yake kwa kuandika mahala ulipochukua kazi hiyo.

Kama inavyojulikana utafutaji wa habari si lelemama na ikumbukwe ili kupata habari iliyo bora na itakayowafurahisha wasomaji wako, kwenda na wakati ni lazima uihangaikie na katika kuihangaikia kuna gharama kibao zinazotumika, ikiwa ni pamoja na usafiri, pesa, na hata mafuta ya gari kutoka mahala Fulani kwenda sehemu nyingine, gharama za simu na hata kuwalipa wale unaowatuma ili kukufanyia kazi hiyo.

Kama umeweza kufanya mambo yote hayo kwa gharama unazozijua wewe uliyeweka stori, ama picha katika Blog yako, halafu watu wenye Blog Fulani wasio na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua kazi yako kana kwamba ameokota tu jalalani na anaweka kwake ili wasomaji wake wasome, bila kuwajulisha kuwa kazi hiyo iliyomvutia imefanywa na mtandao Fulani kwa kweli inaumiza, inaudhi na inarudisha nyuma malengo hasa ya kuwa na mitandao hii, wote tutajaonekana wapuuzi.

Mtandao huu umewavumilia watu hawa kiasi cha kutosha lakini sasa imezidi kukithiri, kwani jamaa hawa wapo katika ukurasa wako kukusubiri kuona tu ulichoweka kwa wakati huo, ili wao wakopi na kupaste kwao, halafu tayari wamemaliza wala hawataki kujihangaisha kufanya kazi ili kuboresha mitandao yao na kuwavutia wasomaji wao.

‘Unapoamua kutangaza vita ujue tayari umeshajipanga kukabiliana na kila litakalotokea mbele yako, na pia umejipanga katika kutoka upinzani wa kweli ili watu waone na wakutambue, lakini sio kwa staili hii ya kuomba mtangaziwe blog zenu kupitia kwa wale walioanza mapema halafu kumbe kazi yenyewe ni kuchukua kazi za watu tu na si kufanya kazi’ yaani kukopi na kupaste,

Kuna msanii mmoja alichoshwa na wenzake wanaotamani kuingia kwenye gemu, lakini wanashindwa kuumiza vichwa kubuni ili kuweza kupata radha tofauti, na kuamua kuwafikishia ujumbe kwa kuwaimba kuwa ‘Si lazima wote tuimbe kuna michezo mingi hata kucheza bao kama huwezi kuimba, ikiwa kila wimbo unaotoka mpya umekopiwa, kama si mashahiri, basi ni Beat,

Na hata katika mablogger si lazima wote tuwe na Mablogger, kama huwezi kuumiza kichwa utoke vipi, basi kaa pembeni waachie wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, kukopi na kupaste hadi mitandao yote inakuwa sawa nini maana ya habari za haraka mtandaoni?,

Huoni kuwa mnawachosha wasomaji wenu, kwa kosoma habari na picha zinazofafa kwa wakati mmoja na katika mitandao yote?,

Tena msomaji wako wakiwa ni waelewa hawawezi kusoma tena mtandao wako kwani habari kama hiyo hiyo walikwishaiona katika mtandao Fulani muda mchache uliopita na dakika chache baadaye wanaikuta vile vile walivyoisoma kwingine ikiwa katika ukurasa wako, mara moja mara mbili msomaji huyo si umempoteza?’’.

Mablogger acheni uvivu na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu, na kama ukifanya hivyo basi jitahidi kumpa credit yule uliyemchukulia kazi yake.

VITU muhimu vy kuwa navyo ili kufanikisha kazi yako ya Blog, ni Laptop ‘Kompyuta mpakato’, ama Desk Top, Modem ‘Internet Wireless’, Kamera hata ndogo tu ya mkononi, na pia ujue maana ya kuanzisha hiyoBlog yako na malengo yako kwa jamii, kwani sidhani kama unaweza kuanzisha blog ili uwe ukisoma mwenyewe na naniliu wako tu.

Na kuwa na kamera si bora tu kuwa kamera pia ujue kuitumia ipasavyo ili kunasa picha nzuri uitakayo na itakayofikisha ujumbe kwa wasomaji wako hata kwa kuiangalia tu, kwa kile ulichokusudia kuwaarifu wasomaji wako.

Baadhi ya Blogs zenye tabia ya kukopi na kupaste orodha yake tayari tunayo na baada ya tangazo hili, zikiendelea tutaziweka hewani ili wasomaji wajue ni Blog ipi ya kweli na ipi ni mamluki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Ni jambo la muhimu sana umelieleza Bwana Michuzi. Ni vyema kutafuta habari zako kama Blogger. Utashangaa na hili Onyo wanalikopi jinsi lilivyo na kuliweka katika Blogs zao pia.

    Gregory.

    ReplyDelete
  2. Umenena mwanawane..kwa kifupi blogs nyingi za bongo ubunifu ni zero..wengi wanachukua news na pc kutoka kwa michuzi..kama kazi hawawezi c waache??Habari michuzi akiweka subiri dkk tano tu blog zote zitatundika hiyo hiyo habari..kuna dada chem kuna cku aliweka hio hio mada kuwa blog nyingi za wabongo ni kucopy na kupaste kwa kwenda mbele...Jamani fanyeni ubunifu kidogo mnatumia nondo hadi kwenye news teehteeh.

    ReplyDelete
  3. You have said it all. Ila mifano ingetusaidia kuwajua wavivu hao

    ReplyDelete
  4. Wengi tumeliona hilo, ushauri kwa picha za blog uziwekee signature yako mfano michuzi etc, nimeliona hili kwa kaka Arnold Kayanda, mara nyingi yeye haibiwi picha zake.

    ReplyDelete
  5. MICHUZI AFADHALI UMESEMA KWA SA BABU WATU WENGI HAWAPENDI KUSHUGHULIKA NA KUHANGAIKA, WANAPENDA EASY JOBS WAKAE TU NA KUTUMIA JASHO LA WENZAO KUJIPATIA UMAARUFU. UMEANZA MBALI NA UNSTAHILI KUFIKA HAPO ULIPO, WENGINE WANAFIKIRI WANAWEZA PANDA UNGO KUFIKA HARAKA LOL WELDONE YOU

    ReplyDelete
  6. Wapo wanao copy mpaka matangazo ya biashara (banners) wakati hawana mikataba na makampuni yanayotajwa kwenye hayo mabango.

    ReplyDelete
  7. Jamani anayelalamika ni www.sufianimafoto.blogspot.com kupitia kwenye blog ya jamii.Ankal yeye 'hanaga' noma, wacopy wasicopy blog ya jamii itaendelea kutesa.

    Ila Sufiani ulichokisema ni kweli,nilishaona na rafiki yangu Mjengwablog analalamikia kitu kama hiki.

    David V

    ReplyDelete
  8. tena memba wa jamii forums ni wezi wakubwa kutwa wapo humu kwa ankali michu wananyofoa picha na kwenda kubandika kule kwao, halafu hawasemi wametoa wapi yani wanaboa sana, kazi kujidai ati huwa hawaingii humu kwa michuzi lakini ndo wezi namba moja, nyie mnaojiita magreat thinker mkija kunyofoa picha na habari huku hasa wewe ctu na wenzako muwe mnasema mmetoa kwa michuzi blog, hapo ndo tutaona ugreat thinker na sio udokozi thinker. na sio kujifanya kuwa nyie ndo sorce ya kila kitu wakati ukweli unajulikana.

    ReplyDelete
  9. SUBIRI SASA SI UMEANZISHA VIJIMAMBO NA CHEKA UNENEPE...BASI SOON WAJASIRIAMALI NAO WATAANZA KUCOPY NA KUPASTE VIJIMAMBO NA CHEKA UNENEPE...BONGO BANAA WEE ACHA TU KWELI NI DASLAMU!!!
    MDAU WA KWA MAMA(QUEEN).

    ReplyDelete
  10. Kaka michuzi that is a crime to steal some material .weka majina hapa tuache kwenda Huko .yaani wabongo hatuna ethics .We need to respect people job duh nomaaa

    ReplyDelete
  11. Take them to court .jamii forum

    ReplyDelete
  12. mimi ni mpenzi wa michuzi,miladayo,shamim,uturn mange,miss jestina,nuru the ligth.mjengwa.sijaona saaana ila wanaweza wakawa wanafanya siku moja moja.ila hao wengine wote walio bakia wanakopi na kupesti kwenu.kama nitakua nimekosea mnisamehe.

    ReplyDelete
  13. Mjomba Michuzi,

    Haiwezekani majasho yanayo churuzika migongoni mwenu yaende bure bure!

    Nafiriki itawalazimu muingie gharama angalau kidogo tu mfanye vitu hivi:

    1.Kusajili kazi zako kwa Patent rights , haki miliki.

    2.Ktk margin za Habari na Picha zako tumia ujuzi wa Graphics ku block picha na habari zako ili ujikinge na wizi!

    ReplyDelete
  14. Blogs za kibongo ni sawasawa tu na bongo fleva.....kukopi kazi za watu na kuziita zao kisha mtu analilia haki ya kazi yake hailindwi.

    ReplyDelete
  15. Poleni,ila yote haya ni matokeo ya "Ujamaa" si tulifundishwa tushirikiane.

    Sasa mbona mna hubiri ubinafsi tena.

    Ila kwa mtazamo wa aliyelalamika ni kama blog zote lazima ziwe za habari kwa picha? Hivi ni sawa?

    ReplyDelete
  16. Staharisha umesikia ???

    ReplyDelete
  17. Hili nalo neno ukiingia blog zote utakuta alichopost Michuzi nao wamepost sio Starlisha peke yake ukiingia blog zote za wabongo wanachukua kazi za kaka Michuzi na tena hao wezi wenyewe ktk mablog yao ndiyo wanajitamba utafikiria wametolea jasho hiyo habari au kutafuta hizo pic.

    ReplyDelete
  18. Mimi naona kama mtu amecopy habari kutoka sehemu furani naona ni njia mojawapo ule ujumbe kusambaa na kumfanya yule mtu wa kwanza kujidai kuwa kazi ameifanya ni nzuri mpaka watu wanaicopy.Mfumo wa kucopy hauwezi kufutika mfano hata wewe hapo ulipo katika CD zako pale nyumbani au Flash ukosi kuwa na nyimbo uliyocopy kutoka mwanamusic hapa dunia mbona ujaenda kukunua orginal copy ili unyanyue kazi ya msanii yule

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...