Sanamu za Tembo juu na chini ya Nyati katika sheli ya Delina Petrol Station kilichopo takriban kilomita moja toka Kibaha ukitokea Morogoro upande wa kushoto. Ubunifu huu umesifiwa sana na wapita njia na kumtaka mwenye sanaa hii aingie hadi miji mingine na kuongeza urembo na pia kutangaza vivutio vyetu vya utalii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Yaani aingie mjini kuchonga hizo sanamu si watu watapanda hao wanyama? Watanzania mnawajuwa ama mnawasikia tu?

    ReplyDelete
  2. Ni nzuri lakini zinachanganya.. mie kwa mara ya kwanza napita barabara ya Morogoro road niliingia hapo nikifikiri naenda kwenye hotel ya kitalii kutahamaki kumbe ni kituo cha mafuta teehteeh na wese nilikuwa nalo basi ikabidi nisepe.. lol

    ReplyDelete
  3. hehehhe yaani nimecheka hadi basi , nimekumbuka hapa shule ya uhuru kwenye round about muheshimiwa meya wa dsm jerry slaa kafanya makosa kuweka ngalawa katika round about ya shule ya uhuru kwani watoto wa mitaani washafanya chumba chao cha kulala , yaani nimecheka kweli ... kakosea kuweka ngalawa pale .... patakuwa gesti bubu pale wewe subiri uone

    ReplyDelete
  4. Kichwa cha habari kingekuwa `UBUNIFU WA KITUO CHA MAFUTA CHA DELINA KIBAHA'

    Shell ni kampuni iliyokuwa kubwa sana hapa Tanzania miaka ya 50 mpaka 80s. Ilikuja kuungana na BP ikajulikana kama BP SHELL hadi mwaka 1985,ambapo BP walibaki kwenye usambazaji na Shell ikajikita kwenye utafutaji wa mafuta(exploration) Watu wa tasinia hii ya habari tujaribu kutumia maneno sahihi ili tusipotoshe vizazi vyetu. Mara nyingi tukirudia kujirekebisha labda tutafanikiwa kwani SHELL ndio kampuni iliyokuwa imejikita sana hapa nchini hivyo kufutika inakuwa ngumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...