Sanamu za Tembo juu na chini ya Nyati katika sheli ya Delina Petrol Station kilichopo takriban kilomita moja toka Kibaha ukitokea Morogoro upande wa kushoto. Ubunifu huu umesifiwa sana na wapita njia na kumtaka mwenye sanaa hii aingie hadi miji mingine na kuongeza urembo na pia kutangaza vivutio vyetu vya utalii
Home
Unlabelled
Ubunifu wa sheli ya delina Kibaha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Yaani aingie mjini kuchonga hizo sanamu si watu watapanda hao wanyama? Watanzania mnawajuwa ama mnawasikia tu?
ReplyDeleteNi nzuri lakini zinachanganya.. mie kwa mara ya kwanza napita barabara ya Morogoro road niliingia hapo nikifikiri naenda kwenye hotel ya kitalii kutahamaki kumbe ni kituo cha mafuta teehteeh na wese nilikuwa nalo basi ikabidi nisepe.. lol
ReplyDeletehehehhe yaani nimecheka hadi basi , nimekumbuka hapa shule ya uhuru kwenye round about muheshimiwa meya wa dsm jerry slaa kafanya makosa kuweka ngalawa katika round about ya shule ya uhuru kwani watoto wa mitaani washafanya chumba chao cha kulala , yaani nimecheka kweli ... kakosea kuweka ngalawa pale .... patakuwa gesti bubu pale wewe subiri uone
ReplyDeleteKichwa cha habari kingekuwa `UBUNIFU WA KITUO CHA MAFUTA CHA DELINA KIBAHA'
ReplyDeleteShell ni kampuni iliyokuwa kubwa sana hapa Tanzania miaka ya 50 mpaka 80s. Ilikuja kuungana na BP ikajulikana kama BP SHELL hadi mwaka 1985,ambapo BP walibaki kwenye usambazaji na Shell ikajikita kwenye utafutaji wa mafuta(exploration) Watu wa tasinia hii ya habari tujaribu kutumia maneno sahihi ili tusipotoshe vizazi vyetu. Mara nyingi tukirudia kujirekebisha labda tutafanikiwa kwani SHELL ndio kampuni iliyokuwa imejikita sana hapa nchini hivyo kufutika inakuwa ngumu.