Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Mh. Dkt. Fenella
Mukangara (mwenye miwani ) leo amepokea taarifa ya kikundi cha Petu Saccos
na kuongea na vijana wa kikundi cha Youth Welding Group cha
Sanawari - Arusha (pichani) alipotembelea na kuangalia jinsi fedha
za mfuko wa vijana zilizotolewa wizara yake zilivyowanufaisha
vijana katika kujikomboa kimaisha na kujiajiri wenyewe.
.Waziri wa Habari , Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Dkt.
Fenella Mukangara (alivaa miwani ) akiongea na wana Saccos wa Petu kupitia
kikundi cha Youth Welding group cha Sanawari mkoani Arusha leo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na . Michezo Dkt. Fenella
Mukangara (kushoto)leo akizungumza na Mjasiriamali Martha Yusuph alipotembelea Soko kuu Saccos Arusha na kuangalia wanufaika
wa mikopo ya mfuko wa vijana uliotolewa na Wizara yake
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara
(kulia) akipata maelezo kutoka kwa mjasiriamali wa Krokon Saccos Asha
Muhamed jinsi alivyonufaika mkopo wa mfuko wa Vijana kutoka Wizara yake .
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella
Mukangara (alievaa miwani) akiongea na wafanyakazi wa TBC na Mafundi wa
Star Times leo alipotembelea Njiro mkoani Arusha kuangalia shughuli
mbalimbali. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
madogo wa welding wanajitahidi, wangepata marketing tools ingekua poa zaidi.
ReplyDelete