Balozi wa Tanzania katika eneo la BENELUX, linalojumuisha nchi za ni Ubelgiji, Uholanzi na Luxemberg Dk Diodorus Kamala amekutana na baadhi ya Watanzania waishio nchini Uholanzi katika safari ya kikazi nchini humo, ambapo kwa pamoja walijadiliana masuala mbalimbali yanoyuhusiana na mustakabali wa uchumi na maendeleo ya Tanzania. 
 Balozi Kamala amewasihi Watanzania hao kuwa wazalendo kwa kutumia utaalamu wao katika kuitumikia nchi katika maeneo mbalimbali yanayohitaji utaalamu hali itakayopelekea kuhakikisha ukuaji wa haraka wa uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. 
Aliongeza kuwa hawana budi kuchangamkia fursa lukuki za uwekezaji kiuchumi zinazopatikana Tanzania. Pia, katika mazungumzo yake na Watanzania hao, Balozi Kamala, amewasihi kuishi kwa umoja na ushirikiano na kuendelea kuipeperusha vyema Tanzania. 
 Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Dorus, uliopo katika Taasisi ya Elimu ya Jamii (ISS), jijini The Hague.
 Mwenyekiti wa TANE, Bw. Kweba Bulemo (aliyesimama Kulia), akisema machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Balozi.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Uholanzi (TANE), Bw. Musuto wa Chirangi  (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Balozi Kamala.
 Balozi wa Tanzania katika eneo la BENELUX, Dk Diodorus Kamala akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi.
 Balozi Dk. Kamala akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Watanzania wa Uholanzi poa sana hakuna mambo ya itikadi za vyama vya siasa. Utaifa mbele, hongera sana Balozi Kamala na viongozi wa Watz Uholanzi. Dumisheni Umoja!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...