TAARIFA YA UHAKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE INAELEZA KUWA JENGO MOJA LA GHOROFA 15 AMBALO NI SEHEMU YA MSIKITI WA SHIA ITHNAASHERI  KATIKA MTAA WA INDIRA GHANDI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM LIMEPOROMOKA MUDA MFUPI ULIOPITA 

INAELEZWA KUWA MPAKA SASA WATU 17 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA WAMEPOTEZA MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA WENGINE WENGI WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.

MKUU WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AKISHIRIKIANA NA WADAU WENGINE WA VYOMBO MBALI MBALI VYA ULINZI NA USALAMA,KUHAKIKISHA UOKOAJI UNAFANYIKA KWA WAKATI.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI DKT EMMANUEL NCHIMBI AMEWASILI PUNDE ENEO LA TUKIO NA INATARAJIWA KWAMBA HATA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ATATEMBELEA SEHEMU HIYO WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA.

CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA JENGO HILO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA,KWANI KILA MTU YUPO KWENYE HEKAHEKA ZA UOKOAJI.

PICHA NA VIDEO ZA TULIO HILO LA KUSIKITISHA ZITAWAJIA PUNDE TU. HIVYO TUVUTE SUBIRA KIDOGO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Inna Lillh wa inna ilayhi rajiuuna.

    ReplyDelete
  2. Inna Lillah wa inna Ilayhi rajiuuna.

    ReplyDelete
  3. Ilikua jengo la NHC? Isiwe wanakimbilia kuboma na kujenga maghorofa kiholela?

    ReplyDelete
  4. ugonjwa wa ujenzi wa majengo feki umeingia rasmi Tanzania! Mungu atunusuru ukizingatia rushwa imetawala kila mahali

    ReplyDelete
  5. Inna lillah lillah wa inna ilayhi rajiun

    ReplyDelete
  6. mtoa kibali anahusu nini na kuwajibishwa si ora utaje wauza nondo na cementi feki?
    hizo kampuni feki kil leo majengo yanaporomoka dar-hatuna hata kifaa cha uokoaji aibu tupu msiba mkubwa haya ndio mambo yanatuvunja moyo sisi watu wa kipato cha chini.

    NA WATU BADALA KUOKOA BASI WANAKWENDA NA MBWA KAMA KUTAIBIWA VILE
    MUNGU AWWALAZE PEMA WALIOFARIKI.AMIN

    ReplyDelete
  7. Inasikitisha sana, na serikali k.m haitakuwa makini yataanguka mengi tu, maana kuna sub-standard vifaa kibao mjini, kwa bei rahisi, na watu mara zote wanakimbilia vitu chee, ili kusevu pesa lakini matokeo ndiyo haya tunayaona na isitoshe kabla ya kupeleka juu gorofa 15 huwa msingi unatathmiwa vizuri kwanza? kazi ipo, na tumuombe Mungu atutetee kwa hili kwa kweli

    ReplyDelete
  8. Mbwa wanasaidia to spot watu waliofukiwa sehemu. This is a serious investigation na kila mtu is a suspect kwanzia mtoa kibali mpk staff, so u gotta think out of the box don't be too critical on things you dont really know.

    Inasikitisha kuona waokoaji taking too long to arrive hapo, mbaya zaidi watu waliopo ktk scene instead ya kuanza to do something to help out wanaleta story tu.

    ReplyDelete
  9. Without Site Investigation, Ground Is a Hazard (Site Investigation in Construction)- Did they follow construction procedures i.e. Materials quality control and Specifications?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...