Home
Unlabelled
kijiwe cha ughaibuni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Huyu jamaa mwenye t shirt ya 'REDDS' anachosema wengi watapinga lakini ni practical na mimi kama diaspora nakubaliana naye. Kama unataka kumsaidia mtu mpe mtaji basi. Misaada ya kutuma hela kila mwezi ndio aina ya misaada inayofanya tanzania ishindwe kuendelea sababu bajeti yetu tunategemea misaada tu! Mpe mtu mtaji ajishughulishe
ReplyDeleteKwa ufupi nyinyi mlivyokueleweni baadhi yenu hamtaki kumsaidia mtu. Hiyo ni tabia za Ughaibuni kwasababu wao wana Welfare na Benefit System. Bongo ujuwe kuwa huku hakuna hayo hivyo benefit system huku ni ndugu, jirani, kijiji. Kwa ufu kama hutaki msaada wa mtu na wewe usisaidie mtu.
ReplyDeleteNi kweli kabisa ukimpa mtu mtaji ajue maisha yake atakavyoyaendesha sio kila siku kuomba omba, ona Tanzania yetu kila siku kuomba pesa nje za misaada na kwenye benki ya dunia, hivi tukizipata zinaenda wapi? au ndio yale yale matumizi yake hayana tija au hayazalishi hivyo tutabakia kuomba mpaka mwisho wa dunia! Mungu atusaidie tubadilike. Kazi nzuri Jabir, Jongo na Ben. Kwa kweli Ben ni chachu hasa kwenye hiki kipindi, na yote usemayo ni kweli tupu. Hata wengine ila Ben ni kiboko hapo. Halafu una akili sana.
ReplyDeletebado nasisitiza kama nilivyokuwa nikisisitiza kwa post nyingi zilizopita hawa jamaa siku zote huwa wanaongea pumba,nia na madhumuni ni kujonyesha wapo nje.jamani huku ughaibuni na sisi tupo pia na mazingira tunayajua bwana.mnadanganya watu mmekuja kula good time!! jama jama! tusidanganyane,unakula good time wakati unakimbiza nahiyo time kwa box?? tena hadi weekend huku ukikimbizana bili? tuwe wa kweli jamaa!! hivi bado mnafikiri bado mtawadanganya wabongo na dunia hii ya utandawazi! at least we mgeni una point lakini huyo yasin na mwaipaja ni pumba tu! kuna siku nilihoji elimu zao leo naomba kipindi kijacho waeleze kazi wanazozifanya marekani,mpaka bw mwaipaja ya kumtia kiburi cha kusema yy na familia yake tu hakuna extended family.bado nasisitiza BONGO NDIO KWENYE MAISHA HUKU UGHAIBUNI KUNA BARABARA NZURI,MAJI NA UMEME WA UHAKIKA!! vinginevyo tusidanganyane!!!
ReplyDeletewewe unaeuliza elimu ya hawa mabwana nadhani uko wrong place. hiki kipindi si cha kitaaluma na ndio maana kinaitwa 'KIJIWE'. Hawa wanajadili maisha kama watu wa kawaida. Wewe kama unataka mambo ya taaluma kuna forum nyingine tafuta kwenye mitandao lakini dhana ya hawa watu ni mambo ya kawaida tu ya maisha na mi naona wanafanya vizuri. Na ndio maana wanakunjwa na Heinneken zao tartiiiiibu....
ReplyDeleteMada nzuri ila ina hitaji umakini,
ReplyDeleteHili la kusema hadi wazazi usiwasaidie kidogo napata shida kuwaelewa.
Kuna point hapa tulio ughaibuni jambo jema ni kuwezesha ndugu zetu kujikwamua kiucumi tena si kumpangia fanya hili lah! mwenyewe akueleze ana taka kufanya nini na atoe mchanganuo!Kwa hapo foleni western union itakoma.
Jipangeni zaidi si siku nyingi wasiowakubali watawakubali!
kijiwe akihitaji elimu hayo mambo wanoyoyaongea elimu tosha kwa sababu mambo yanayofanyika kuhiyo kijiwe mko juu
ReplyDeleteNYIE MNAOSAPOTI KUPELEKA MISAADA HUKO BONGO NAHAKIKA HAYAJAWAKUTA YA KUWAKUTA. KIKWETE MWENYEWE ALISEMA HATA MAMA YAKO ANAWEZA KULA HELA YAKO ULIYOTUMA ILI UJENGEWE,KWAKIFUPI KAMA KUNA NAMNA NI KUWAWEKEA KIJISHUGHULI CHA KUWAINGIZIA THEN WEWE UNAENDELEA NA MAISHA YAKO. TATIZO NYUMBANI WATU SI WAKWELI
ReplyDeleteWe Mdau wa Tue Mar 12, 09:32:00 pm 2013:
ReplyDeleteUnasema wanasema [wa]"nakula good time wakati unakimbiza nahiyo time kwa box??" Yaani kweli wewe mtu na akili zako unafikiria ukifika Marekani ni maraha tu hamna kazi? Marekani jamaa wanafanya kazi sana lakini ikifika wikend wanajirusha vile vile. Nawaomba wabongo wenye mawazo mgando kama haya mpate bausara mnatia aibu. Halafu mmekazana wapiga box. Ndiyo tatizo letu kubwa wabongo tunadharau kazi za wenzetu. Ndiyo maana wanafunzi kibao wamefeli kwa vile waalimu hawaheshimiki, vile vile mji wa Dar es salaam mchafu kwa vile wale akina mama wanosafisha taka taka hawaheshimiki hata kidogo. Mtu apige Box aokote taka taka kwani kuna ubaya ghani kama analipwa vizuri?!! Kwa Marekani, jamaa wanaokusanya taka taka wanalipwa vizuri na wakati wakutumia hela yao hakuna mtu anae muuliza aliipataje hiyo hela. Bongo tuamke tuache longo longo zisizo na tija. Kwenye hiki kijiwe jamaa wanatoa maoni mazuri kusadia jamaa Bongo waelewe hali inavyokuwa wakati mwingine, lakini jamaa wengine humu kwenye maoni wantoa maoni na kama chuki fulani ndani yake. Maisha kila mtu na bahati yake, tusikate tamaa.
Huyo anayeuliza elimu za wanakijiwe nadhani yeye aulizwe elimu yake kwa sababu bado ajazipata point na madhumuni ya kijiwe. Kwenda shule si kuelimika!
ReplyDeletekweli nakipenda hichi kijiwe ni shule tosha kwa watu wanaodhani ndugu zao wakiwa marekani au nchi yeyote basi wao ni kujibweteka hawatafuti namna ya kujikwamua nikukaa tu na kutegemea ndugu aliyeko ulaya atatuma pesa utafiki huku kuna machimbo ya pesa hawajui methali isemayo mtegemea cha nduguye hufa masikini kweli hawa watu walio na ndugu nje ya nchi wanatesa sana ndugu zao pasipo huruma yaani kama kukomoana
ReplyDelete