MAREHEMU SAMSON AMOS MITULA.
SITAWEZA KUISAHAU KAMWE TAREHE 22.03.2003 SIKU TULIPOKUWA SAFARINI NAWE TOKA DAR ES SALAAM KWENDA SINGIDA NA TULIPOFIKA CHALINZE TULIPATA AJALI MBAYA SANA UKANIACHA SIJITAMBUI.BAADA YA WIKI MBILI NIKIWA NAHOJI SANA KWANINI HAUJI KUNISALIMIA INGAWA PIA SIKUWA NIKIJUA NAUMWA NINI HADI JOPO LA MADAKTARI WALIPONIAMBIA KUWA HAUKO NASI TENA DUNIANI TANGU TAREHE 22.03.2003, KWAMBA TULIPATA AJALI MBAYA SANA CHALINZE NA ULIFARIKI DUNIA PALEPALE HAKIKA ILINIUMA SANA.
SIKU NILIPOPEWA TAARIFA HIZO NDIPO NILIPOJUA KUWA NAMI NINA BANDEJI NYINGI USONI.NI MIAKA KUMI(10) SASA TANGU UTUACHE KAKA YETU MPENDWA,MIMI ERASTO YOHANA SIMA NA FAMILIA YANGU TUNAKUKUMBUKA SANA TUTAZIDI KUYAENZI MEMA MENGI ULIYOTUACHIA.
UNAKUMBUKWA SANA NA MKE WAKO MPENZI MWL FAITH SAMSON KIDASHARI WATOTO WAKO WOTE HASA LILIAN ULIYEMWACHA AKIWA NA UMRI WA MWEZI MMOJA TU,WAZAZI WAKO BW & BIBI AMOS MITULA,FAMILIA YOTE YA MZEE KIDASHARI,DADA ZAKO,KAKA ZAKO,SHEMEJI ZAKO,WADOGO ZAKO,RAFIKI ZAKO WOTE NA WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA,HAKIKA TUTAKUKUMBUKA DAIMA KAKA SAM.
BWANA ALITOA NA BWANA AKATWAA JINA LAKE LIBARIKIWE AMEN
ERASTO YOHANA SIMA
MKUU WA WILAYA BARIADI-SIMIYU
What a touching story. RIP brother
ReplyDeleteUpumzike kwa amani
ReplyDeletePumzika kwa aqmani, nasi tu nyuma yako, tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi.
ReplyDeleteJina la Bwana Libarikiwe
Pole sana Erasto, its a very touching message..... RIP Samson
ReplyDeleteErasto habari za kifo cha kaka yako kimenigusa sana asante kwa kushare habari hiyo ya ajali, mungu azidi kuwatia nguvu mpate kuwalea vyema watoto wa kaka Samson kwa mapenzi makubwa kama ishara ya kumuenzi marehemu
ReplyDelete