MAREHEMU SAMSON AMOS MITULA.

SITAWEZA KUISAHAU KAMWE TAREHE 22.03.2003 SIKU TULIPOKUWA SAFARINI NAWE TOKA DAR ES SALAAM KWENDA SINGIDA NA TULIPOFIKA CHALINZE TULIPATA AJALI MBAYA SANA UKANIACHA SIJITAMBUI.BAADA YA WIKI MBILI NIKIWA NAHOJI SANA KWANINI HAUJI KUNISALIMIA INGAWA PIA SIKUWA NIKIJUA NAUMWA NINI HADI JOPO LA MADAKTARI WALIPONIAMBIA KUWA HAUKO NASI TENA DUNIANI TANGU TAREHE 22.03.2003, KWAMBA TULIPATA AJALI MBAYA SANA CHALINZE NA ULIFARIKI DUNIA PALEPALE HAKIKA ILINIUMA SANA.

SIKU NILIPOPEWA TAARIFA HIZO NDIPO NILIPOJUA KUWA NAMI NINA BANDEJI NYINGI USONI.NI MIAKA KUMI(10) SASA TANGU UTUACHE KAKA YETU MPENDWA,MIMI ERASTO YOHANA SIMA NA FAMILIA YANGU TUNAKUKUMBUKA SANA TUTAZIDI KUYAENZI MEMA MENGI ULIYOTUACHIA.

UNAKUMBUKWA SANA NA MKE WAKO MPENZI MWL FAITH SAMSON KIDASHARI WATOTO WAKO WOTE HASA LILIAN ULIYEMWACHA AKIWA NA UMRI WA MWEZI MMOJA TU,WAZAZI WAKO BW & BIBI AMOS MITULA,FAMILIA YOTE YA MZEE KIDASHARI,DADA ZAKO,KAKA ZAKO,SHEMEJI ZAKO,WADOGO ZAKO,RAFIKI ZAKO WOTE NA WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA,HAKIKA TUTAKUKUMBUKA DAIMA KAKA SAM.

BWANA ALITOA NA BWANA AKATWAA JINA LAKE LIBARIKIWE AMEN

ERASTO YOHANA SIMA

MKUU WA WILAYA BARIADI-SIMIYU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. What a touching story. RIP brother

    ReplyDelete
  2. Pumzika kwa aqmani, nasi tu nyuma yako, tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi.
    Jina la Bwana Libarikiwe

    ReplyDelete
  3. Pole sana Erasto, its a very touching message..... RIP Samson

    ReplyDelete
  4. Erasto habari za kifo cha kaka yako kimenigusa sana asante kwa kushare habari hiyo ya ajali, mungu azidi kuwatia nguvu mpate kuwalea vyema watoto wa kaka Samson kwa mapenzi makubwa kama ishara ya kumuenzi marehemu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...