Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Sabyasachi Kar, wakati
alipotembelea kujionea mashine za kusaga mawe, zilizopo Kijiji cha
Sabasaba Irimba, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani
Mara, iliyo sambamba na Uwekaji jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya
Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi
Musoma, leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na Mbunge wa Butiama Vijijini, Nimrod Mkono, baada ya
kusikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Sabyasachi Kar, kuhusu mashine za
kusaga mawe wakati alipotembelea kuona mashine hizo, zilizopo Kijiji cha
Sabasaba Irimba, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani
Mara, iliyo sambamba na Uwekaji jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya
Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi
Musoma,leo.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...