Ankal akiwa katika mazishi ya mwanachama mwandamizi wa Klabu ya Saigon ya jijini Dar es salam Marehemu Mrido aliyefariki juzi. Marehemu, aliyezikwa leo mchana katika makaburi ya Mwinjuma, Magomeni, jijini Dar es salaam huku mvua kubwa ikinyesha, atakumbukwa kuwa mmoja wa wanachama wakereketwa wa Yanga na pia mlezi wa timu ya mpira wa miguu wa vijana wa enzi hizo wa Kariakoo ya Jugnu Mehu iliyokuwa kama Yosso ya Saigon wakati Mchikichi Boys ilikuwa mdogo wa Jugnu
Jeneza likitolewa kwa ajili ya mazishi yaliyohudhuriwa na vijana na wazee wa mjini pamoja na wanachama wa Klabu ya Saigon
Waombolezaji kaburini
Viongozi wa Klabu ya Saigon wakisimamia mazishi hayo
Makaburi ni ya Mwinyimkuu Mshindo,Magomeni Mapipa,Wilaya ya Kinondoni,DSM.
ReplyDelete