Mtaalamu wa kutoa damu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mpango wa Damu Salama, Linus Kupuya akimtoa damu mmoja wa waumini wa Kanisa la Adventista Wasabato, Dolka Juma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Huduma na Matendo ya Huruma kwa Jamii Ulimwenguni. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni wiki.
WAUMINI wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania
wameungana na waumini wenzao ulimwenguni kusherehekea siku ya huduma na matendo
ya huruma kwa jamii ambayo yaliadhimishwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Idara
ya Vijana Jimbo la Mashariki mwa Tanzania Mchungaji, Emmanuel Sumwa alisema
kanisa hilo lilipanga kuwa siku hiyo iwe siku ambayo waumini wake wakisaidiwa
na idara ya vijana kutoa huduma za
kijamii kwa jamii inayowazunguka.
“Kwa kuzingatia umuhimu wa siku hii waumini wa kanisa duniani
kote wametembelea maeneo mbali mbali kwa ajili ya kutoa misaada kwa wahitaji
ikiwa ni pamoja na kuchangia damu katika benki ya Damu salama, kutembelea hospitali,
kutoa misaada kwa wagonjwa, kutembelea vituo vya watoto yatima, kituo cha
kijiji cha watuwasiojiweza Msimbazi center, mahabusu ya watoto upanga na
magereza,” alisema.
Mchungaji Sunwa alitaja maeneo yaliyotembelewa kuwa ni Mwananyamala, Muhimbili, Amana,Temeke, Lugalo, Nevy, Parestina,
Mbwenimission, Ocean Road, Vijibweni Kigamboni, Mabagala Zakiena, Tumbi Kibaha, Dar group na vituo
vya watoto yatima Bunju,Ungindoni na mburahati.
Pia mchungaji huyo aliwataka Watanzania kuwa na moyo wa
kujitolea pale panapohitajika hasa kwa watu wasiojiweza na watoto wanaoishi
katika mazingira magumu.



ReplyDeleteSindano ni ndogo lakini inaogofya kweli kweli ... You can see from the body language of these people
http://machithela.blogspot.com/
hakuana cha "anasitizya"?
ReplyDeletehawa wataalamu wa afya nadhani hawajui kuchoma sindano. Haiwe zekani watu wale wanaumia hivyo kwa utoa damu tu.
ReplyDeletehuyo jamaaa hapo juu,namfananisha na mtu nilisoma naye sengerema sekondari,miaka ya 1985 na kuendelea alikuwa anaitwa Jeradi mapigi,sikjui ndiye?
ReplyDeletehongera adventists
ReplyDeletetarehe 15-3-2014 maadhmisho hayo yatafanyika tena.wabarikiwe waadventista kote duniani.
ReplyDelete