Punde waumini takribani bilioni 2 wa Kanisa Katoliki ulimwenguni watapata kiongozi  mpya.
A). Je ni nani wanamchagua?
Kuanzia jumanne jioni  tarehe 12/03/2013, idadi ya Makardinali 115 wa kanisa Katoliki kutoka sehemu mbalimbali duniani wameingia katika “conclave” ndani ya kanisa dogo maarufu kwa jina la Sistine tayari kwa shughuli hiyo nyeti kabisa ambayo itawachukua siku kadhaa. Awali ilitarajiwa Makardinali 117 kati ya 153 wenye sifa za kumchagua kiongozi huyo wa juu wa kanisa hilo wangefika makao makuu Vatikani kwa shughuli hiyo. Lakini kutokana na sababu za kiafya, Kardinali emeritus  Julius Ruyadhi DARMAATMADJA ,sj kutoka Jarkata, Indonesia hakuweza kufika kwa sababu za kiafya, na Kardinali Keith O’Brien, ex- Cardinal toka Ediburgh, Scotland hakufika kwa sababu zake binafsi.
Hivyo watakaojisogeza katika “boksi” kumchagua kiongozi huyo ni 115 wenye umri chini ya miaka 80.
B). Mgawanyo unaenda hivi:
Bara la Ulaya linawakilishwa na makardinali 60; wakitokea : Italia pekee ni : 28. Ujerumani: 6.Uispania: 5. Polandi: 4. Ufaransa: 4. Austria: 1. Ubelgiji: 1. Uswisi: 1. Ureno: 2. Uhaolanzi: 1. Ireland: 1. Jamuhuri ya Czech: 1. Bosnia-Herzegovina: 1. Hungary: 1. Lithuania: 1. Kroatia:1. na Slovenia ni 1.
Bara la Amerika ya Kusini, maarufu pia kama Latino Amerika ni Makardinali 19; Wakitokea : Brazil: 5. Mexico: 3. Argentina: 2. Kolombia: 1. Chile: 1. Venezuela: 1. Jamuhuri ya Dominikan : 1. Cuba: 1. Honduras: 1. Peru: 1. Bolivia: 1. na Ecuador ni 1.
Bara la Amerika Kaskazini hasa Marekani ni Makardinali 14 ; wakitokea:  Marekani ni: 11. na Kanada:  ni 3.
Bara la Afrika litawakilishwa na Makardinali 11: wakitokea Nigeria: 2. Tanzania: 1. (Polycarp PENGO, Askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar-es-Salaam, Tanzania). Afrika ya Kusini : 1. Ghana: 1. Sudan: 1. Kenya: 1. Senegal: 1. Misri: 1. Guinea: 1. Na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ni : 1
Na bara la Asia litawakilishwa na makardinali 10: wakitokea India: 4. Ufilipino: 1. Vietnam: 1. Indonesia: 1. Lebanon: 1. China: 1. na Sri Lanka: 1.
Kati ya Makardinali 117wenye kupiga kura, 67 waliteuliwa na Papa Benedikti wa XVI. Wanaobakia 50 waliteuliwa na Papa John Paul II. --Kati ya hao walio hai ni 6 na ndiyo pekee  walikuwepo wakati wa Mtaguso wa pili yaani tunaweza kuwaita  (Council Fathers at the Second Vatican Council) nao ni Makardinali Angelini, Arinze, Canestri, Delly, Fernandes de Araújo, na Lourdusamy). Na waliosalia wana zaidi ya miaka 80 na hivyo hawataingia katika hiyo “Conclave”. -- Kati ya makardinali walio hai leo, 99 walishiriki katika uchaguzi wa mwaka 2005. Kati yao  49 tyari wana zaidi ya miaka 80 hivyo hawataweza kumchagua Papa mpya. (Baba mtakatifu Benedikti wa XVI naye alikuwa kati ya walioshiriki uchaguzi wa 2005.)
C). WANAOPIGIWA CHAPUO.
Ikumbukwe kuwa viongozi hao walikutana Vatican ambako ni makao makuu ya Kanisa hilo na kuzungumzia maswala mbalimbali yanaloligusa kanisa na waumini wake. Kwa nyakati mbalimbali Makardinali hao walielezea maswala mbalimbali yanayoligusa Kanisa hilo kutoka katika maeneo yao.
Katika hali la “kuwachora” au kuwasanifu” jamaa kutoka kusini mwa jangwa la  sahara, ambapo waandishi na watu mbalimbali wamekuwa wakiwadadisi kama kiongozi huyo atatokea bara hilo watajisikiaje. Sikatai kuwahoji mawazo na fikra pia maoni yao ni vizuri. Lakini katika hali ya ukweli  walikuwa wakiwa“chora” tu maana kwa sasa mtazamo na wakati wa kupata kiongozi toka ukanda huo unaonekana wazi kuwa bado wakati wake haujaiva. Pengine inawezekana maana ni kazi ya Roho Mtakatifu.
Wadadisi, watetesi  wa mambo na vyanzo mbali mbali vinatabiria na kubashiri kuwa huenda majina haya yakatoka ndani ya “Conclave” hiyo kama Baba Mtakatifu, kiongozi wa kanisa hilo. Hii ni kwa mpangilio wa chagizo hizo.
1). K. ANGELO SCOLA, (71) Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Milan, Italia.
2). K. ODILO PEDRO SCHERER, (63) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Sao Paulo, Sao Paulo, Brazil.
3). K. MARC OUELLET, (68) kiongozi mkuu mstaafu wa Maaskofu katika Roma, maarufu kama “Prefect Emeritus of the Congregation for Bishops” ni Askofu mkuu wa jimbo la Quebec, Canada-Francophonie.
4). LUIS ANTONIO TAGLE, (55) Askofu mkuu wa jimbo la Manila, Ufilipino. Ndiye kijana wa pili kwa umri mdogo. Wadadisi wa mambo wanatabiri pia anaweza kuwepo kwenye uchaguzi ujao kama kandidate wa uongozi huo. 5). K. FRANCISCO ROBLES ORTEGA, (64) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Guadalajara, Jalisco, Mexico. 6). K. CHRISTOPH SCHÖNBORN, (68) Askofu mkuu wa jimbo la kuu la Vienna, Austria. 7). K. JORGE MARIO BERGOGLIO, (76) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Buenos Aires, Argentina. 8). K. SEAN PATRICK O’MALLEY, (68) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Boston, Massachusetts, USA. 9). K. PETER ERDO, (60) Askofu mkuu wa jimbo kuu l’Esztergom-Budapest, Hungary. 10). K. ALBERT MALCOM RANJITH PATABENDIGE DON, (64) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Colombo, Sri Lanka. 11). K. TIMOTHY MICHAEL DOLAN, (63) Askofu mkuu wa jimbo kuu la New York, New York, USA. 12). K. TELESPHORE PLACIDIUS TOPPO, (73) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Ranchi, India. 13). K.  JOAO BRAZ de AVIZ,  (65) Askofu mkuu wa zamani wa jimbo kuu la Brasilia, Brazil. Sasa anafanya kazi Vatican, Rome. 14). K. FERNANDO FILONI, (66), Italia,  Kiongozi wa ofisi ya  uinjilishaji makao makuu Vatican. 15). K. Leonardo SANDRI, (69) Argentina, Anafanya kazi makao makuu Vatican.

D). WAKATI KANISA LIKIKUWA ZAIDI NCHA YA KUSINI, UONGOZI UNABAKI KWA KIASI KIKUBWA HAPA ULAYA.
Zaidi ya karne moja iliyopita ukuaji wa kanisa, idadi ya waumini inaongezeka nje ya bara Ulaya na sasa kuna wastani wa zaidi ya waumini milioni 200 wa kanisa Katoliki wapo katika bara la Latini-Amerika ukilinganisha na Ulaya. Ukiangalia kwa makini Makardinali toka bara la Ulaya wanakaribia nusu ya wapiga kura wote. Ikumbukwe kuwa ili kumpata baba mtakatifu, inatakiwa achaguliwe na zaidi ya kura 77 ; kati ya 115.

Tunaona bara la Amerika ya Kusini ndilo bara lenye wakatoliki wengi kuliko mabara mengine. Afrika inaonyesha kuendelea kukua kwa kasi kwa kuwa na idadi ya waumini wa kanisa hilo. Bara Asia linaonyesha kuendelea kuongeza idadi ya waumini wakanisa hilo kwa siku za usoni. Kwa Afrika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiyo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya Wakatoliki ikifuatiwa na Nigeria ya tatu ikiwa ni TANZANIA ikifuatiwa na Uganda kwakaribu kabisa. Halafu Angola inafuatia huku Kenya ikifuatia.
   
Imeandaliwa na Frédéric Meela, Paris 
kwa msaada wa vyanzo mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwa Tanzania hakuna data zinazoonyesha idadi ya watu kulingana na dini yao; uwe makini mwandishi. Serikali haijafanya hiyo sensa ya aina hiyo tangia mwaka 1967. Nimetoa maoni haya kwa kueleweshana ili tuandike kitu cha kweli na tujenge taifa kwa kufanya kitu kilicho cha kweli. Scientifically proved

    ReplyDelete
  2. Akipatikana Pope kutoka chini ya Jangwa la Sahara /Afrika, nadhani Waumini wa Katoliki wa Afrika watakesha usiku kucha wakisali huku wanalia!

    ReplyDelete
  3. Uchambuzi mzuri kabisa lakini ikumbukwe tu kuwa Baba mtakatifu (papa) si mwakilishi wa bara, ukanda au taifa bali ni mwakilishi wa Kanisa zima. Pia haongozi peke yake. Anawashauri na waratibu wengine wakaribu.

    Wakatoliki tunaimani dhabiti kuwa ni chaguo la Mungu. Hivyo yeyote atakayechaguliwa ni atakuwa mwakilishi wa Kristo na kiongozi wa wote.

    ReplyDelete
  4. Kitu kinachochekesha Waingereza katika sensa yao wameonyesha mpaka dini, race, na wapi wanakoishi watu wa ana mbali mbali.

    ReplyDelete
  5. Anonymous No 1.Kwa taarifa yako Wakatoliki idadi yao hufamika,Kupitia makusanyo(data)mbalimbali ambazo Mama Kanisa huzi hifadhi,Mf;Kupitia register ya Ubatizo kwa waumini wake,Taarifa za Kila "Kigango/jumuiya
    Vifo,Komunio,kipaimara,ambapo kila parish huwa responsible katika hilo na jedwali hili hufahamika nakuthibitishwa JIMBONI na kufanyiwa kazi,kwa mantiki hiyo basi sisi wakatoliki twajijua katika hilo!(scientific proved)

    ReplyDelete
  6. anony wa Wed Mar 13, 04:55:00 pm 2013 kungekuwa na button ya like ningekugongea! baelezee!

    ReplyDelete
  7. Yes kuhesabiwa waumini wa kikatoliki si jukumu la serikali, ni makanisani na data zipo za idadi ya waumini kama Anonn wa Wed Mar 13, 04:55:00 pm 2013 alivyosema. so kumjibu mdau wa kwanza hapo juu.

    ReplyDelete
  8. Idadi inasemwa ni wakatoliki idadi yao katika nchi moja dhidi ya nchi nyingine sio dhidi ya dini zingine annoy wa kwanza unachemka sana usiwe na jazibaaa, wakatoliki wote wanaandikwa pindi wanapobatizwa, pia wanafutwa pindi wanapofaliki kupitia jumuia ndogo ndogo (familia zisizozidi 15) zinaishi na kusali na kusaidiana pamoja takwimu zao wapeleka hadi roma itali, mwandishi hajaandika toka dar es salaam yupo itali na hajui sensa ya tanzania na pia hajui dini yako POLE SANA.

    ReplyDelete
  9. mwandishi hajakosea

    yeye katoa ranking za africa ,hakuzungumzia madhehebu mengine ya ukristo wala didni nyingine.

    yaweza kuwa hoa wakatoliki ni wachache kulinganisha na madhehebu mengine ,

    pia yaweza kuwa idadi ya waumini wa didni nyingine inaongezeka kwa kasi kubwa kuliko wakatoliki,

    hivyo hakuna haja ya ubishi katika maelezo yaliyotolewa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...