Mtumishi katika mnara wa Canton, mrefu kuliko yote nchini China na watatu duniani kwa urefu, Sarah Xie, akimuonyesha mandhari ya jiji la Guangzhou, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Kinana na ujumbe wake walipopanda hadi mwisho mnara huo wenye urefu wa zaidi ya futi 100, Machi 13, 2013. Wengine Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine shigella. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakitazama maumbo ya mandhari ya mji wa Guanzhou, China, yaliyopo ndani ya mnara wa Cnton wenye urefu wa zaidi ya mita 100, walipotembelea mnara huo, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi, Yussuf Mohamed Yusuf wakitaza bidhaa zinazouzwa kwenye kilele Mnara wa Canton ambao ni mrefu kuliko yote nchini China ukiwa na urefu wa zaidi ya mita 100, mjini Guangzhou, China. Dk. Asha-Rose Migiro na Yusuf ni miongoni mwa viongozi walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CCM mnaona jinsi Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wanavyoongoza mapinduzi ya kiuchumi China kwa vitendo?

    Sasa tunangojea Kigoma iwe Dubai ya maeneo ya Maziwa makuu Afrika Mashariki na Kati kabla ya 2015.

    Mdau
    Pwani ya Ziwa Tanganyika, Tanganyika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...