Ndugu zangu wapendwa nawasalimu katika jina la alie juu yeye atupae uzima. Naomba niwajulishe watz wote waishio UK kuwa ndugu yetu Josephat Torner alieshiriki katika BBC Documentary ya albino killings in Tanzania iliyoonyeshwa mwaka jana ameshawasili tokea jana tayari kushiriki katika film nyingine itakayoonyeshwa siku ya Ijumaa tarehe 15 Mach 2013.
Josephat Torner angependa sana kukutana na Watanzania waishio huku nje ili atueleze uzito wa hili swala Na jinsi tutakavyoweza kisaidiana. Tunawaomba watanzania tujitokeze kwa wingi tumuunge mkono huyu ndugu yetu kwa jitihada zake na ujasiri wake kwani ni kazi inauohitaji moyo sana na inaumiza roho sana kusikia mateso wanayoyapata hawa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
Filmed over six years, In the Shadow of the Sun tells the story of two men with albinism in Tanzania, Josephat Torner and 15-year-old Vedastus, who are pursuing their dreams in the face of virulent prejudice. Through his intimate portrait, filmmaker Harry Freeland reveals a story of deep-rooted superstition, heartfelt suffering, and incredible strength.
Please note: All Human Rights Watch Film Festival screenings will start promptly at the advertised time.
SHOWING AT:
SOHO CURZON
FRIDAY 15 MARCH 2013
TIME: 18:30
ADVISED 16
Safi sana,zipatikane nakala za kiswahili kwa ajili ya TV za nyumbani TZ
ReplyDeleteUjumbe kwa wanaoua au kuwatoa viungo walemavu wa ngozi:Hivi kama mlemavu wa ngozi ni mtoto wako,mume/mke wako,baba/mama yako,mjomba,shangazi,jamaa,mpenzi/rafiki n.k na huu unyama akafanyiwa mmoja wa hao niliowataja hapo juu utasikiaje uchungu(feeling)??
Nilikuwa nimekaa na fariki zangu siku moja,rafiki zangu wa mataifa ya nje.Tupo nje ya nchi...basi katika gumzo,mmoja akaanza kutueleza kama Utani vile "Nimesoma jana kwenye internet kumbe Tanzania watu wanaua walemavu wa ngozi kwa imani za Kishirikina ,hivi ni kweli"?Nikafikiria haraka haraka sana nijibu vipi(sijui nikubali au nikatae),nilijisikia kama mimi ndiye nawaua manake nilikuwa mtanzania peke yangu!.Mnaoishi huko nje ya nchi mnaweza kunipinga-UNAPOKUWA NJE YA NCHI UNAFARIJIKA SANA UKISIKIA WATU WANAIPA SIFA NZURI TANZANIA.
David V