Utalii wa wenzetu kwenye zoo moja huko Budapest Hungary ambapo watalii wanawekwa kwenye Canter lenye wavu na kuanza kuzunguka maeneo ya wanyama. Je wadau wanaonaje magari ya utalii nyumbani Tanzania pia yangekua na wavu kama huu?
Chef Issa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. South Africa nao wana magari ya namna hii ingawa ya kwao ni makubwa zaidi.

    Ignorant

    ReplyDelete
  2. Utalii wa kwenye zoo kweli, lakini kule mbugani ambako hujui simba yuko wapi inabidi lifanyiwe improvement kidogo.

    ReplyDelete
  3. Tutaunda tume ifanye uchunguzi wa kina na kuona usalama wa watalii utakuwaje,tume itafanya ziara ya mafunzo ili tuagize magari maalum toka kiwandani kwa kuzingatia mapendekezo ya tume.

    ReplyDelete
  4. Hapa simba ndio wanatalii binadamu walikua kwenye ZOO(caged)

    ReplyDelete
  5. hayo ni mazingira ya ZOO. Kwenye mbuga halisi ya wanyama inaweza kuwa hatari na watalii wataogopeshwa badala ya kuvutiwa. Njia inayokubalika kupeleka watalii kwa ukaribu zaidi na wanyamama kwenye mazingira halizi ni kutmia baloon inayopaa angani. Kama tahadhani tu ni kwamba mambo mengi ya wanyama kama simba na chui mnayoona Ulaya Marekani msichukulia kwa uhalisi sababu hao wanyama wengi walitolewa Afrika wakiwa wadogo na kukuzwa kama ajili ya maonesho kwa hiyo hawana uhalisi kama wale wa mbugani (eg wale mnaowaona kwenye circus shows).

    ReplyDelete
  6. Oh God the one with a cap on... Gosh, I wish I could get my paws on him!!!! Ningemlaje????

    ReplyDelete
  7. halafu wanyama wenyewe wanakuja chukua kwenye nchi zetu na wanatushinda maarifa

    ReplyDelete
  8. Yaani najisikia kama kitoweo. Mdau, CA, USA

    ReplyDelete
  9. Huko ni kutamani kukutana na mola wako mapema.mimi hunipandishi gari ng'o!

    ReplyDelete
  10. Huu ni kama ukatili wa wanyama.
    Hii ni kama vile mtu akuletea pilau ndani ya chupa na huna uwezo wa kafungua hiyo chupa.
    They should get out and shake hand with their hosts.
    Ibrahim

    ReplyDelete
  11. Hii ni salama zaidi, maana kule Fresno, California Marekani Mhudumu wa Zoo alishambuliwa na simba tarehe 7 Machi ,2013.

    ReplyDelete
  12. hii imekaa poa bro!hebu tanzania na sisi tuzinduke basi!vipi,tumerogwa?tuwe wabunifu na options na packages mbalimbali!utalii upo wa mambo mengi sana sana,lakini,hatuzitumii rasilimali tulizo nazo!hiyo picha nimeipenda,just imagine,wavu huo upasuke ghafla,itakuwaje hapo?nini kitatokea kwa ndugu zangu hao waliopo ndani ya cage?kuna mtu atakumbuka Camera yake au Wallet iko wapi au Girlfriend wake yuko wapi?au itakuwa mshikemshike,kila mtu akiinusuru roho yake?suppose you had a girlfriend with you in that cage,and suddenly,a mighty Lion breaks loose part of that cage,and manages to enter into it,tell me,what will you do under the circumstances?will you embrace your girlfriend in order to protect her life?or will you run for your life and girlfiend "baadaye?",such thrills is what makes that tour even more wanting!

    ReplyDelete
  13. Pamoja na wavu huo wa kukinga hatari, Mnyama ni mnyama licha ya kuwa Klabuni kwetu Msimbazi bado mambo si shwari ni kuwa simba halowani hata akinyeshewa na mvua.

    Wana Yanga na Michuzi wenu inabidi muwe jasiri mkiwa ndani ya magari ya wavu kwa kuwa mnakabiliana na mnyama Simba ana kwa ana,,,kama hapo kwenye picha mnavyoona!


    Kama hapo ndani mpo Wana Yanga nadhani wapo watakao jikojolea kwa woga vile simba kudandia juu hapo.

    Mnyama mchezo?

    ReplyDelete
  14. !?????!!!We mdau hapo juu unaetuhabarisha kuwa South Africa nao wana magari ya namna hii,hoja haikuwa nani na nani wana magari ya namna hii,alichoshauri mtoa hoja kwa njia ya picha ni kuwa kuna haja na sisi kuwa na magari ya aina hii bila kujali ni ya ukubwa kiasi gani.Wadau tusipende kukurupuka na kuanza kubofya bila ya kutafakari kwanza na kuelewa mada/hoja

    ReplyDelete

  15. Hahahahaa duh hii noma huu ni utalii au kutiana presha tu kazi kweli kweli

    ReplyDelete

  16. HII KALI BWANA SAFI TU EMBU NA MAKAMPUNI YA UTALII TZ WAJARIBU, ILA INATAKA MOYO

    ReplyDelete
  17. Bongo hapa cku wavu ukiwekwa sub standard itakuwa ahueni kwa wanyama. free meal served on skewers

    ReplyDelete

  18. Huu utalii au kurushana roho duh!!

    STATES

    ReplyDelete

  19. NIMEIPENDA HII, ILA INATAKA MOYO SANA TU

    ReplyDelete

  20. Hahahahaaaa duh hii kweli au uzushi? cheki watu wote wamejikusanya sehemu moja sasa simba akizunguka huko walikojikusanya si kazi tena ukiangalia juu yupo inamaa watu watachuchumaaa tehe tehe hii kiboko mi naona kama hatari sana na watu hawana amani huko maana simba mate yanawadondoka na wanakwarua hizo nyavu.

    MDAU BELGIUM

    ReplyDelete
  21. Mvua je na jua je? acha tubaki na Ma-long base/chasis yetu Landrovers!

    ReplyDelete
  22. wewe unafikiri simba wa Africa ni sawa na Simba wa ulaya? sisi Simba Wetu Wanafanana na akili zetu, akiona gari kama hilo na nyie mpo ndani lazima achane nyavu achomoke na mtu. kamwe msifikirie kuleta magari kama hayo!

    ReplyDelete
  23. Good but hatari

    machithela.blogspot.com

    ReplyDelete
  24. Gari zetu si mnazijua, ikiharibika kama hapo itakuwaje?

    ReplyDelete
  25. nafikiri sio mbaya lakini kwa tanzania wangejaribu magari makubwa kama kuanzia tani 7

    kwa upande mwingine naona kama ni hatari zaidi kwa usalama wa hao binadamu
    imekuwa kama vile hao binadamu ndio wanyama wamefungiwa
    na hao wanyama ndio binadamu wapo free wanaangalia binadamu waliofungiwa

    sasa hapo ni wanyama wanatalii kwa kuangalia binadamu

    kwa upande mwengine ni hatari kwa sababu hilo gari likitokea lolote labda kuwaka moto au kupinduka ina maana watakuwa wamejijengea kaburi maana kuokoa maisha yao itakuwa kazi kubwa maana wamejifungia.

    ReplyDelete
  26. Uwiiiiiii! me ntakufa kwa kihoro kabla hata ya kutalii nusu saa

    ReplyDelete
  27. Gari zetu spana mkononi, je likiharibika itakuwaje?

    ReplyDelete
  28. hapa naona wanyama wanatalii na binadamu wamefungiwa wasije wadhuru wanyama
    Brain

    ReplyDelete
  29. Aisee, Mimi nadhani hapo ningeshatokwa na samadi muda mrefu.

    Mwanamalundi wa JF

    ReplyDelete
  30. Hii inaongeza kivutio zaidi. Nasisi tucopy na kupaste.
    Mdau asante kwa kutuongezea maarifa

    ReplyDelete
  31. Ni idea murua! Ila hawa simba ni wa ki-bagradeshi (Soft lion). Simba wa bongo ni balaha.Wanataka magari makubwa kama ya south africa

    ReplyDelete
  32. kWANI LAZIMA MAGARI YA UTALII YAFANANE NA Hungary!Hapo ndipo roho zetu kwatu kwakuwa tumefanana na ulaya.

    Hamajona magari ya utalii TZ.Kaoneni kwanza ndipo mutoe maoni.Si kila siku MKUBWA KAMA TEMBO!.

    ReplyDelete
  33. Yanga S.C endeleeni kuhemea matumboni kwa woga mbakie humo humo ndani na msitoke, mashabiki hamuamini kama mpo salama humo ndani mnatetemeka ndani ya Tundu la ndege.

    Mkitoka tu, mmeraruliwa na mmeliwa na Mnyama Simba S.C!

    Na hapo hapo msimamo wa Ligi unabadilika na Simba inakuwa kileleni !!!

    ReplyDelete
  34. Wanatamani kweli minofu ya ndani ya gari!

    ReplyDelete
  35. Hilo la juu sijui linataka kuwakojolea?

    ReplyDelete
  36. Namuunga mkono anonymus wa 09:58:00am 2013. Lakini kabla ya kuunda tume, kwanza kamati ya bunge itafanya ziara maalum ya kutembelea maenro husika na ikishajiridhisha ndipo iundwe tume
    kuona usalama wa watalii utakuwaje,nayo tume itafanya ziara ya mafunzo na kisha itapendekeza uundwaji wa kikosi kazi kitakachotoa mapendekezo ya namna ya uagizaji wa magari hayo maalum toka kiwandani kwa kuzingatia hali halisi ya wakti tulionao.

    ReplyDelete
  37. Kila kitu Kamati ,kila Kitu kamati!

    Ama kweli Bongo tambarale, itatokea mtu amepoteza simu yake ya mkononi si pia ataomba iundwe Kamati?

    ReplyDelete
  38. Huyo simba hapo juu akiamua kujisaidia itakuwaje??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...