Jengo lililo pembeni mwa msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi katikati ya jiji la Dar es salaam linavyoonekana baada ya kuporomoka asubuhi hii. Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova kawaambia wanahabari kuwa kila aliyehusika na ujenzi, usimamizi na hata utoaji vibali atawajibishwa endapo kutaonekana kumekuwepo uzembe upande wake
Taharuki kila mahali katika eneo la tukio
Jengo limetapakaa barabarani
wananchi wakishuhuria kwa huzuni
Bango la wakandarasi
Hassan Mhelela wa BBC alikuwa miongoni mwa wanahabari wa kwanza kufika eneo la tukio
Moja ya magari kadhaa yaliyodondokewa na kifusi
Gari ingine ambayo inasemekana ndani yake mna watu
Ulinzi wa kutosha kila pembe


Hii ndiyo faida ya RUSHWA kila kona tutasingizia kazi ya MUNGU
ReplyDeleteKifo hakikosi sababu kila sekunde viumbe. vinakufa na viumbe vinazaliwa kazi ya muumba hiyo ndio siku yao imefika sisi tujiandae safari ni yetu sote wao wametangulia sisi tunafata nyuma
DeleteHiyo ni Jengo la NHC za joint venture?
ReplyDeleteankali umezidi kushabikia vikwangua anga sasa unaviona vikwangua anga vyako vinaanza kukwangua ardhi kwa kurudi chini
ReplyDeleteujenzi mbovu sana wahusika wasipoangalia kuna hatari kama hizo kutokea sana baada ya miaka 20 zile cement na vifaa vitakavyokwisha nguvu katika majengo mengi marefu ya hapo dar es salaam
mungu walaze pema peponi waliotangulia siku ya leo hii
ameen ameen ameen.
Kwa kweli tusipokuwa makini na haya maghorofa ambayo wenyewe tunayaita "yanaota kama uyoga" tutaangamiza wengi!!
ReplyDeleteWamiliki wa haya majengo nao wanachangia sana kadhia kama hizi; wako loose mno!
Anyway haya tutayajadili baadae sasa hivi tuzidishe nguvu katika kuokoa majeruhi.
Mwenyezi Mungu atujalie wepesi katika kazi hii.
MUNGU WALAZE PEMA PEPONI
ReplyDeleteRUSWA
TAMAA YA PESA
HAKI NDOGO
NDO VINAWAUWA MASIKINI
WATANZANIA SASA TUJIULIZE UZALENDO WETU UKO WAPI? HAKI YETU IKO WAPI?
MATAJIRI WENYE NMADARAKA WANATOA VIBALI VYA UJENZI NA WANAJUA KABISA NYUMBA BILA MSINGI HAISIMAMI HAYA HAYATOKEI KTK NCHI ZA WENZETU
Poleni sana ndugu zangu!
ReplyDeleteCHUMA YETU TUPELEKE CHINA; SISI TUJENGE KWA UDONGO!
ReplyDelete