Jengo lililo pembeni mwa msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi katikati ya jiji la Dar es salaam linavyoonekana baada ya kuporomoka asubuhi hii. Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova kawaambia wanahabari kuwa kila aliyehusika na ujenzi, usimamizi na hata utoaji vibali atawajibishwa endapo kutaonekana kumekuwepo uzembe upande wake
 Taharuki kila mahali katika eneo la tukio
 Jengo limetapakaa barabarani
 wananchi wakishuhuria kwa huzuni
 Bango la wakandarasi

 Hassan Mhelela wa BBC alikuwa miongoni mwa wanahabari wa kwanza kufika eneo la tukio
 Moja ya magari kadhaa yaliyodondokewa na kifusi
 Gari ingine ambayo inasemekana ndani yake mna watu
 Ulinzi wa kutosha kila pembe
Bila vifaa vizito kazi inakuwa ngumu

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hii ndiyo faida ya RUSHWA kila kona tutasingizia kazi ya MUNGU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kifo hakikosi sababu kila sekunde viumbe. vinakufa na viumbe vinazaliwa kazi ya muumba hiyo ndio siku yao imefika sisi tujiandae safari ni yetu sote wao wametangulia sisi tunafata nyuma

      Delete
  2. Hiyo ni Jengo la NHC za joint venture?

    ReplyDelete
  3. ankali umezidi kushabikia vikwangua anga sasa unaviona vikwangua anga vyako vinaanza kukwangua ardhi kwa kurudi chini

    ujenzi mbovu sana wahusika wasipoangalia kuna hatari kama hizo kutokea sana baada ya miaka 20 zile cement na vifaa vitakavyokwisha nguvu katika majengo mengi marefu ya hapo dar es salaam

    mungu walaze pema peponi waliotangulia siku ya leo hii

    ameen ameen ameen.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli tusipokuwa makini na haya maghorofa ambayo wenyewe tunayaita "yanaota kama uyoga" tutaangamiza wengi!!
    Wamiliki wa haya majengo nao wanachangia sana kadhia kama hizi; wako loose mno!
    Anyway haya tutayajadili baadae sasa hivi tuzidishe nguvu katika kuokoa majeruhi.
    Mwenyezi Mungu atujalie wepesi katika kazi hii.

    ReplyDelete
  5. MUNGU WALAZE PEMA PEPONI

    RUSWA
    TAMAA YA PESA
    HAKI NDOGO
    NDO VINAWAUWA MASIKINI
    WATANZANIA SASA TUJIULIZE UZALENDO WETU UKO WAPI? HAKI YETU IKO WAPI?
    MATAJIRI WENYE NMADARAKA WANATOA VIBALI VYA UJENZI NA WANAJUA KABISA NYUMBA BILA MSINGI HAISIMAMI HAYA HAYATOKEI KTK NCHI ZA WENZETU

    ReplyDelete
  6. Poleni sana ndugu zangu!

    ReplyDelete
  7. CHUMA YETU TUPELEKE CHINA; SISI TUJENGE KWA UDONGO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...