IDADI ya wasanii wa nje watakaokuja kutumbuiza kwneye Tamasha la Pasaka mwaka huu imezidi kuongezeka na sasa Wanyarwanda nao wamethibitisha kushiriki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee Yesu imethibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
“Watakuja kung’arisha tamasha la mwaka huu na wamejipanga vya kutosha kuhakikisha mashabiki wanapata burudani ya nguvu, nia yetu ni kuwa na wasanii wakubwa Afrika na hilo ndilo tutakalolifanya mwaka huu.“Kabla ya Jumatano tutatangaza msanii mkubwa mwingine ambaye bado tunaendelea na mazungumzo naye kuhakikisha mambo yanakuwa safi, ili aje kutumbuiza kwenye tamasha letu,” alisema Msama.
Alieleza kuwa katika albamu yao hiyo ina nyimbo nane ambazo ni JY’ Ushima Uwite, Mtegee Yesu, Ndifuza Kugerayo, Iyana Iby’ Isi, Yesu Niwe Mungeri, Parapanda, Abasaruzi na Nenda.Wasanii wengine wa nje ya Tanzania ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hili ni , Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya. Wasanii wa Tanzania ni Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu.
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
|
Home
Unlabelled
Wanyarwanda kutumbuiza Pasaka Dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ila hiyo picha hakuna mwimbaji hata mmoja wa Ambassadors of Christ labda mtuambie ni kwaya nyingine tutawaelewa.
ReplyDeleteAma kweli huu Muungano wa Afrika ya Mashariki una faida sana!
ReplyDeleteLicha ya wengi wetu kuogopa EAC ina faida zake!!!, wajameni angalieni hamuoni watoto hao?
Mdau wa kwanza,
ReplyDeleteBongo imekuwa New York Dunia nzima imeshajua tumeingia kwenye utajiri wa Gas na Oil hivyo Bongo sio kama tunavyoidharau sisi wenyewe ipo juu.
Unaweza kusikia baadaya kutumbuiza hao wooote wamezama Mitaani hawataki kuridi kwao!
anony no 1. Wote walio kwenye picha ni waimbaji wa Amassadors of Christ. Ila simuoni Sarah hapo wajameni.....
ReplyDeleteAnany wa Mon Mar 11, 06:09:00 am 2013, angalia vizuri picha toka kushoto wa kwanza, tatu, sita, saba na wa mwisho. Hao wame-appear mara nyingi. Kwani jina la kwaya ni sura za watu au ni waimbaji kwa ujumla hata kama kuna sura mpya?kama ni hivyo Msondo Ngoma isingekuwepo mpaka leo.
ReplyDeleteYaelekea huwafahamu au una matatizo ya macho. Hao ndio wenyewe
ReplyDeleteKaribuni sana nyumbani,hapa ni kwenu pia!Nyimbo zenu nazikubali sana,Mungu awabariki ili mshinde vikwazo!Kazi mnayo ifanya ni Takatifu,inaeneza neno la kuponya uzima!Amani pamoja nasi,amen!Karibuni sana Tanzania!mdau wenu wa Mwanza.
ReplyDelete