Mtaalamu wa kutoa damu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mpango wa Damu Salama, Dk. Abdu Juma  akimtoa damu mmoja wa waumini wa Kanisa la Adventista Wasabato, John William ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Huduma na Matendo ya Huruma kwa Jamii Ulimwenguni. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Picha Habari Mseto Blog)

Mtaalamu wa kutoa damu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mpango wa Damu Salama, Linus Kupuya akimtoa damu mmoja wa waumini wa Kanisa la Adventista Wasabato, Dolka Juma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Huduma na Matendo ya Huruma kwa Jamii Ulimwenguni. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni wiki.

WAUMINI wa Kanisa la Waadventista wa  Sabato Tanzania wameungana na waumini wenzao ulimwenguni kusherehekea siku ya huduma na matendo ya huruma kwa jamii ambayo yaliadhimishwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Jimbo la Mashariki mwa Tanzania Mchungaji, Emmanuel Sumwa alisema kanisa hilo lilipanga kuwa siku hiyo iwe siku ambayo waumini wake wakisaidiwa na idara  ya vijana kutoa huduma za kijamii kwa jamii inayowazunguka.
“Kwa kuzingatia umuhimu wa siku hii waumini wa kanisa duniani kote wametembelea maeneo mbali mbali kwa ajili ya kutoa misaada kwa wahitaji ikiwa ni pamoja na kuchangia damu katika benki ya Damu salama, kutembelea hospitali, kutoa misaada kwa wagonjwa, kutembelea vituo vya watoto yatima, kituo cha kijiji cha watuwasiojiweza Msimbazi center, mahabusu ya watoto upanga na magereza,” alisema.

Mchungaji Sunwa alitaja maeneo yaliyotembelewa kuwa ni Mwananyamala, Muhimbili, Amana,Temeke, Lugalo, Nevy, Parestina, Mbwenimission, Ocean Road, Vijibweni Kigamboni, Mabagala Zakiena, Tumbi Kibaha, Dar group na vituo vya watoto yatima Bunju,Ungindoni na mburahati.

Pia mchungaji huyo aliwataka Watanzania kuwa na moyo wa kujitolea pale panapohitajika hasa kwa watu wasiojiweza na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa


  1. Sindano ni ndogo lakini inaogofya kweli kweli ... You can see from the body language of these people
    http://machithela.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. hakuana cha "anasitizya"?

    ReplyDelete
  3. hawa wataalamu wa afya nadhani hawajui kuchoma sindano. Haiwe zekani watu wale wanaumia hivyo kwa utoa damu tu.

    ReplyDelete
  4. huyo jamaaa hapo juu,namfananisha na mtu nilisoma naye sengerema sekondari,miaka ya 1985 na kuendelea alikuwa anaitwa Jeradi mapigi,sikjui ndiye?

    ReplyDelete
  5. hongera adventists

    ReplyDelete
  6. tarehe 15-3-2014 maadhmisho hayo yatafanyika tena.wabarikiwe waadventista kote duniani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...