Mgeni Rasmi katika Hafla ya Siku ya Wanawake,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisoma hotuba fupi mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofayika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni mwelekeo wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimisha Machi 8 Duniani kote.
 Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akisalimiana na mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwenye hafla ya Women's Celebration 2013 iliofanyika leo jijini Dar.
Muandaaji wa hafla ya Women's Celebration 2013 kutoka kampuni ya 8020 Fashions, Shamim Mwasha akipongezwa na Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda kwa kazi nzuri alioifanya ya kufanikiwa kuwakusanya wanawake wenzake na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na maendeleo kwa ujumla,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi 8 Duniani kote.
 Mwimbaji mahiri wa miondoko ya taarab nchini,Khadija Kopa akitumbuiza mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya  wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.


KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA
AU
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mambo ya mitandao hayo tukio linafanyika mnaliona muda huo huo asante michuzi

    ReplyDelete
  2. HONGERA SANA SHAMIMU. TUNAKUSHUKURU KWA KUTAFUTA NJIA YA KUWAUNGANISHA WANAWAKE. NINA IMANI NA WANAWAKE.

    ReplyDelete
  3. Hapana bwana , wanawake mtabaguana mpaka lini? hii haikujulikana kwa wanawake wote . Ina maana wanawake wa Tz ni wale wake wa viongozi na wale wanaofahamika tuuuu?

    Hata wanawake waliopewa uongozo hili hawalioni.

    Ndio maana wanawake huwa na mawazo yale yale hayabadiriki sabb ya kukutana wale wale . Kuna mawazo mazuri yanabaki bila kufanyiwa kazi . Nyie mnabaki na Oh mke wa waziri fulani, mke wa balozi fulani...Hii ni mpaka lini?

    Ndio tunaamini kuwa kuna mambo amabyo kundi la watu fulani wanapaswa kukaa pamoja lkini si ki hivi. wanawake Tz MMEBUGI MEEN

    ReplyDelete
  4. wanawake wa tanzazai tuko JUU kama mawingu, uliyebugi ni wewe usiekuwa na taarifa hii kitu imetangangazwa zaidi ya miezi sita nyuma kupita vyombo vya habari vyote, na kweli wanawake tulihamasishana sana ili tumuunge mkono shamim kwa kutafuna siku ya kutuunganisha wanawake. sasa hao wake wa viongozi tulikuwa nao tukajumu tukala na kucheza pamoja kama wanawake wenzetu na si wake.
    WAMAWAKE OYEE Ukweli siku ya jana nilifurahi sana mungu akuzidishie shamim akupe umri na mwakani ufanya kubwa kuliko hii.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa March 4 07:59:00 wewew ndiyo unataka kuwatenga wanawake. Hili tangazo lilikuwa kwenye vyombo mbali mbali kwa karibu mwezi mzima na halikubagua mtu, sasa wewe ulitaka waandaaji wafanyeje? Kuhusu kufunguliwa na mke wa waziri fulani, je ukusika Chausiku binti Fulani atafungua huu mkutano unadhani nani atakwenda wakati huyo Chausiku hajulikani? Kuna sababu wafunguzi wa mikutano ni watu wanaojulikana.
    Kidogo kidogo tutafika hii nayo ni hatua tulikuwa hatuna hata kitu kama hiki bali vigenge vigenge ambavyo navyo havikuwa imara. Wanawake ndiyo uti wa mgongo wa familia zetu na hatimaye taifa letu. Women Do matter.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...