Mgeni Rasmi katika Hafla ya Siku ya Wanawake,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisoma hotuba fupi mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofayika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni mwelekeo wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimisha Machi 8 Duniani kote.
Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akisalimiana na mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwenye hafla ya Women's Celebration 2013 iliofanyika leo jijini Dar.
Muandaaji wa hafla ya Women's Celebration 2013 kutoka kampuni ya 8020 Fashions, Shamim Mwasha akipongezwa na Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda kwa kazi nzuri alioifanya ya kufanikiwa kuwakusanya wanawake wenzake na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na maendeleo kwa ujumla,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi 8 Duniani kote.
Mwimbaji mahiri wa miondoko ya taarab nchini,Khadija Kopa akitumbuiza mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.







mambo ya mitandao hayo tukio linafanyika mnaliona muda huo huo asante michuzi
ReplyDeleteHONGERA SANA SHAMIMU. TUNAKUSHUKURU KWA KUTAFUTA NJIA YA KUWAUNGANISHA WANAWAKE. NINA IMANI NA WANAWAKE.
ReplyDeleteHapana bwana , wanawake mtabaguana mpaka lini? hii haikujulikana kwa wanawake wote . Ina maana wanawake wa Tz ni wale wake wa viongozi na wale wanaofahamika tuuuu?
ReplyDeleteHata wanawake waliopewa uongozo hili hawalioni.
Ndio maana wanawake huwa na mawazo yale yale hayabadiriki sabb ya kukutana wale wale . Kuna mawazo mazuri yanabaki bila kufanyiwa kazi . Nyie mnabaki na Oh mke wa waziri fulani, mke wa balozi fulani...Hii ni mpaka lini?
Ndio tunaamini kuwa kuna mambo amabyo kundi la watu fulani wanapaswa kukaa pamoja lkini si ki hivi. wanawake Tz MMEBUGI MEEN
wanawake wa tanzazai tuko JUU kama mawingu, uliyebugi ni wewe usiekuwa na taarifa hii kitu imetangangazwa zaidi ya miezi sita nyuma kupita vyombo vya habari vyote, na kweli wanawake tulihamasishana sana ili tumuunge mkono shamim kwa kutafuna siku ya kutuunganisha wanawake. sasa hao wake wa viongozi tulikuwa nao tukajumu tukala na kucheza pamoja kama wanawake wenzetu na si wake.
ReplyDeleteWAMAWAKE OYEE Ukweli siku ya jana nilifurahi sana mungu akuzidishie shamim akupe umri na mwakani ufanya kubwa kuliko hii.
Mdau wa March 4 07:59:00 wewew ndiyo unataka kuwatenga wanawake. Hili tangazo lilikuwa kwenye vyombo mbali mbali kwa karibu mwezi mzima na halikubagua mtu, sasa wewe ulitaka waandaaji wafanyeje? Kuhusu kufunguliwa na mke wa waziri fulani, je ukusika Chausiku binti Fulani atafungua huu mkutano unadhani nani atakwenda wakati huyo Chausiku hajulikani? Kuna sababu wafunguzi wa mikutano ni watu wanaojulikana.
ReplyDeleteKidogo kidogo tutafika hii nayo ni hatua tulikuwa hatuna hata kitu kama hiki bali vigenge vigenge ambavyo navyo havikuwa imara. Wanawake ndiyo uti wa mgongo wa familia zetu na hatimaye taifa letu. Women Do matter.