Msanii chipukizi wa Injili hapa nchini Eveline Kabwelile anategemea kuachia albamu yake ya kwanza aliyoibatiza jina la YESU KOMANDO yenye jumla ya nyimbo tisa aliyoirekodi katika studio ya Iki Production chini ya Producer Iki

1. Yesu komando
2. Ananitosha bwana
3. Mungu hawezi kukusahau
4. Nakupenda mokozi
5. Mshukuru Mungu
6. Ni wewe mwenyewe
7. Usinipite Mokozi
8. Mokozi asifiwe
9. Ni nani

Albamu hiyo inategemewa kuzinduliwa tarehe 12 may 2013 katika Kanisa la Hollyness pentecote kwa Mchungaji Ndalima Ubungo kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.

Akizungumzia sababu hasa iliyomfanya kuingia kwenye uimbaji wa Nyimbo za injili Eveline amesema kwa upande wake anasukumwa sana na wito wa Mungu kwani nilianza kupenda kuimba toka nikiwa mdogo na iko kwenye damu, yake

“Nilianza kuimba toka nikiwa mdogo sikumbuki ni mwaka gani, albamu hii nimeanza akuiandaa 2010 na 2011 ndio nikaanza kurekodi audio za nyimbo zangu na nilianza kurekodi video za nyimbo zangu mwaka 2012 katika studio Brayanz work chini Byayan Hasani na nyimbo zote zimeshakamilika audio na video tayari kwa uzinduzi”

Albamu ya audio na video ya albamu Yesu Komando itaanza kuuzwa siku ya uzinduzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kosa la jinai kuvaa nguo za kijeshi?

    ReplyDelete
  2. Mhhhh!jamani,nimetafuta maneno ya kuandika lakini nikakosa,nachoweza kusema hatua tuliyofikia ya kutumia jina la bwana wetu mwokozi kupitia injili katika kufanikisha malengo fulani binafsi ya kimaisha inatia wasiwasi kama kweli hizi nyimbo za injili ni za kumtukuza bwana wetu yesu kristo au kuna malengo fulani nyuma yake.

    ReplyDelete
  3. Unaimba nyimbo za injili halafu una vaa military style?
    Sijui ;)
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  4. kibiashara zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...