KUNA HALI YA HATARI SANA KATIKA ENEO LA KITUO CHA POLISI KAWE JIJINI DAR ES SALAAM HIVI SASA BAADA YA WANANCHI KUAMUA KUKIVAMIA KITUO HICHO KUTOKANA NA DEREVA MMOJA WA BAJAJI KUDAIWA KUUWAWA NA ASKARI WA JESHI LA WANANCHI AMBAYE ANASHIKILIWA NA POLISI.

KIUKWELI HALI NI MBAYA SANA ENEO HILI HIVI SASA KWANI MABOMU YA MACHOZI NA MILIO YA RISASI VIMETAWALA KATIKA ENEO HILI IKIWA NI KATIKA HALI YA KUWATAWANYA WANANCHI HAO AMBAPO WANANCHI HAO WANAENDELEA KURUSHA MAWE.
 BARABARA YA IMEFUNGWA NA HAKUNA SHUGHULI ZINAZOWEZA ENDELEA KUFANYIKA KATIKA ENEO HILO.
 MOSHI WA MABOMU YA MACHOZI UKIONEKANA KWA MBALI WAKATI POLISI WAKIENDELEA KUWATAWANYA WANANCHI HAO.



WANANCHI WAKIWA WAMEJIKUSANYA PEMBENI WAKITAFAKARI KINACHOENDELEA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Polepole jamii ya Watanzania tunauhalalisha utamaduni Wa kujichukulia sheria mkononi kwenye tukio. Mungu na atunusuru

    ReplyDelete
  2. hao wajesh wamezidi kuonea raia

    ReplyDelete
  3. Watanzania ni kama vile nyasi kavu sana za kiangazi, jua likizidi kupita kiasi tu basi zinawaka moto, Watu wamechoka na ufisadi na wanahasira hasira kama wendawazimu vile, wnatafuta sababu yeyote ile ili wafanya vurugu, wengine ndo wanajipatua riziki at the same time, bongo arosto, tutamkumbuka mwalimu.

    ReplyDelete
  4. Problem ni unemployment - hawa vijana hawana kazi ndiyo maana wanaleta fujo every where. It is hard to justify the existence of a whole Ministry of Youth - what its rol?

    ReplyDelete
  5. Badala ya kuachia vyombo vya usalama, wasio na kazi wanaingilia kati!

    ReplyDelete
  6. Haya ndio madhara ya umaskini maana wanaona kama wenye magari wanawaibia ndio maana wanafunga barabara. Tukio hili halihusiani na barabara ila wana hasira na "matajiri" na hapo mtu akipita na gari lazima watamshambulia ingawa hausiki na tatizo lao.

    ReplyDelete
  7. Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wotee nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana weeee

    chonde chonde vyombo husika vya dora tunawaomba mpunguze hasira na kujali raia wema

    hivi watanzania siku hadi siku wanazidi kuzoea milio ya bunduki na mabomu tofauti na hapo zamani

    nakumbuka zamani ukisikia sauti ya bunduki unakimbilia nyumbani kujificha

    wakuu wa dora mnapowapeleka watanzania ni kubaya zaidi maana mnawazoesha kinguvu mazoea ya vurugu na milio ya bunduki na mabomu

    hayo mazoea yatakuja kuleta hatari zaidi siku za mbeleni kwani watanzania tukishakuwa hatuogopi bunduki wala mabomu ndio mwanzo mbaya

    kuna hatari ya kuja kupambana kwa mapigano kati ya vyombo vya dora na raia wema

    tunawaomba wahusika msimamie suala hili kwa nguvu zote

    tudumishe amani nchini kwetu wengi wanaililia nasi tusichezee

    wakuu msilale kabisa kwa mambo kama haya tuonyesheni jitihada zenu kukomesha maonevi

    kila mtanzania ana haki sawa ya kujivunia nchi yake na kupata huduma kama mtanzania mwingine

    sasahivi wananchi raia wema wamechoshwa kabisa na tabia za kuonewa

    Elimu duni kwa mlalahoi
    Matibabu duni kwa mlalahoi
    Usafiri duni kwa mlalahoi
    Ndoto za kuwa na maisha mazuri kwa mlalahoi zimeisha.


    Mungu ibariki tanzania wabariki raia wema wa tanzania waangamize viongozi mafisadi na wenye roho mbovu kwa raia wema.

    ReplyDelete
  8. Kiini cha matatizo likiwemo hili na la kuchunja kuwezesha kitoweo mezani ni Umaskini huu mkubwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...