Pichani kati ni mratibu wa filamu ya Love & Power Bwana Myovela Mfwaisa akizungumza na Wanahabari Mapema leo jijini dar.
Dar
es Salaam, 10th April 2013
Imetayarishwa
na Kanumba the Great Film , ikiongozwa na Steven C. Kanumba imeandikwa na Ally Yakuti.
Ile filamu ya Love
& Power ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa filamu hatimaye
mwisho wa wiki hii siku ya Ijumaa tarehe 12th April 2013
itazinduliwa na kuingia sokoni rasmi na kusambazwa nchi nzima na kampuni ya
mahiri ya usambazaji wa filamu ya Steps
Entertainment Ltd.
Akizingumza na waandishi wa wanahabari mratibu wa
filamu ya Love & Power Bwana
Myovela Mfwaisa amesema kuwa “Filamu ya Love & Power ni filamu ya mwisho kutengenezwa na marehemu The
Great Kanumba inaingia sokoni na
kuwafikia watanzania wote siku ya ijumaa,”
Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wa tasnia ya
filamu na watanzania wote kwa ujumla na kuweza kujionea kazi bora
iliyotengenezwa na gwiji la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya
Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania, kila mpenzi wa filamu aweke ahadi
kutokuikosa filamu bora na ya mwisho kuigizwa na marehemu nyota wa filamu
Tanzania.
Akizungumzia kwa ufupi juu ya filamu ya Love & Power Bwana Myovela, “Filamu
ya Love & Power imetengenezwa na
kampuni ya Kanumba the Great film kwa kushirikia na Steps Entertainment Ltd ikiwa
imeandikwa na Ally Yakuti, Filamu ya Love & Power imeshirikisha wasanii
nyota katika tasnia ya Filamu Tanzania kama Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’,
Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth
Bosco ambaye ni mdogo wake na marehemu kuongozwa na Steven Kanumba, Watayarishaji
wakuu ni Steps Entertainment Ltd imetengenezwa
hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo
tofauti tofauti.
Lugha iliyotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili
lakini pia Lugha ya kiingereza imetumika kama ‘Subtitles’.
Umri wa kutazama filamu ya Love &
Power ni miaka 16 ni filamu nzuri inayotazamwa na watoto pamoja na familia,
iliyopewa kibali cha ukaguzi Kutoka Bodi
ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza Tanzania.
Katika kuhakikisha kuwa wasanii wanafaidika na kazi
zao tunaomba kila mdau wa filamu awe mlinzi wa kazi hizi za filamu za
kitanzania kwa kupambana na Maharamia wa kazi za Wasanii wa filamu, pia
tunawaomba wapenzi wa filamu kununua nakala halali yenye nembo ya Steps Entertainment Ltd, hiyo
itachochea maslahi kwa wasanii wa Tanzania na kuongeza ajira kwa vijana ili
kufikia hilo nunua filamu ya Love &
Power halali.
Unaweza kupata filamu ya Love & Power kwa kuwasiliana na Wasambazaji kwa namba hizi: 0716
788 805, 0713 570 581
Asanteni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...