Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli. akiongea leo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo lilikoporomoka ghorofa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo, akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka. 

Kamati hiyo imeziamuru halmashauri za Wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni kufanya tathmini ya majengo yote na kuchukua hatua mara moja zitapogundulika zimejengwa chini ya kiwango.
Tayari watu 11 wanaotuhumiwa kuhusika katika ujenzi wa ghorofa lililoporomoka wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kuua bila kukusudia 
 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka akiwa eneo la jengo lilioporomoka. Nyuma yake ni jengo ambalo linajengwa na mjenzi yule yule aliyejenga liliporomoka. Kamati hiyo imetoa siku nne kwa mjenzi kubomoa jengo hilo ambalo linasemekana nalo limejengwa chini ya kiwango. 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk TerezyaHuvisa wakimsikiliza   Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka  na  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli akijadili jambo na Bw. Azim Dewji pamoja na mjumbe wa kamati Mhe Zakhia Meghji. Picha na mdau Sujit Bhojak

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kuuliza si ujinga jamani naomba niulize kwamba wakati hiyo gorofa inajengwa, huyo waziri wa ardhi na kundi lake zimaa lilikuwa waapi? na kuna utaratibu wowote wa kukagua ujenzi kamla haujafanyika? au ndo rushwa imetawala wana pewa kitu kidogo wana nyamaza na kuangalia pembeni? mie naomba wahusika waanze kujiuzulu haraka haraka, na wachukuliwe sheria. asanteni mungu awabariki woote.

    ReplyDelete
  2. Haya hayaa mafanikio ya rushwaaaa.magorofaaa yote yaliojengwa tanzania haiwezi ukalinganisha roho ya mtu mmoja.

    ReplyDelete
  3. Jee unatarajia Waziri apite akikagua majumba yote ya mjini, na Manispaa watafanya nini?

    Ni wajibu wake pale panapotokea tatizo ndiyo aingilie kati na hao wengine wafuatilie kikawaida.

    Na ndiyo maana wale waliowajibishwa walikuwa wanahusika moja kwa moja na ukaguzi wa majengo hayo

    ReplyDelete
  4. mama tibaijuka jiuzuru kesi kama hii ungekuwa nchi za maendeleo ilikuwa wewe wa kwanza kufikishwa kizimbani. na mjengo wa mamarwakatare umepewa sikungapi kuvunjwa nanini kinachofanyika mpaka sasa. tunaomba majibu.

    ReplyDelete
  5. "Livunjwe ndani ya siku nne" hii ni kauli ya kisiasa zaidi. Je walishafanya impact assessement and cost benefit analysis-jinsi ya kubomoa ilo jengo? Nina hamu kuangalia utekelezaji wake.

    ReplyDelete
  6. Kuanzia sasa jengo linalo zidi ghorofa kumi lazima kibari toka kwa waziri kama kweli unataka kudhibiti ujinga la sivyo yanakuja mengi tu kubomoja in few yrs to come madame!msimamizi wa kazi anashida ya maisha na mjezi ana pesa chafu hapo rushwa inakosekanaje???mshahara wake ni mbovu na malipo ya rushwa ni mara kumi ya mshahara wake hapo utawezaje kukosa majengo mabovu?

    ReplyDelete
  7. IN DA UK, WE CALL THIS KNEE JERK REACTION.

    ReplyDelete
  8. Mdau hapo juu nakubaliana na wewe mia ya mia. Muheshimiwa mama Tibaijuka ana mengi ya kujibu. yeye kama waziri wa ardhi ameusika vipi katika kuelewa ujenzi wa hilo gorofa lililoua watanzania wenzetu? hapo tunapoongea kuna mtoto aliye poteza baba, kaka au dada kwenye hilo jengo, this is very serious! Naona majengo yoote yaliyo marefu yakaguliwe haraka sana. Hatuwezi kupoteza maisha ya watu kijinga kijinga namna hii. Asante sana. Michuzi Oyeee

    ReplyDelete
  9. Ni uzembe kwenda mbele. Kwani tayari naona law suit nyingine hiyoo...Kwa hakika mwenye jengo anafurahia kuwa jamaa wacha wavunje na atawapeleka mahakamani. Na mtaona mwenye jengo hatalivunja mwenyewe. Mwisho wa siku na serikali itatakiwa liable kumlipa fidia. Lile la masaki aliloliboa Lowasa mbona wamelipa fidia jamaa mabilioni ya kutisha.

    ReplyDelete
  10. MIMI NAON SERIKALI HAIFUATI MIPANGILIO YA KUWEKA MAMBO SAFI NA SALAMA SIO TU KWA UJENZI BALI KILA KITU MPAKA ITOKEE AJALI. JANA WANACHUNGUZA MATAIRI YA MH. JAJI ALIYEFARIKI KTK AJALI..MROROGORO TOKEA MBEYA??? DAWA ZA FEKI, VITU VYA VIWANGO VYA CHINI VINAPITA BANDARINI ALAFU WAKAVIKAMATE MOROGORO NA KUCHOMA???
    LAKINI JAMBO LILILONISHANGAZA NI KWA WAZIRI KUAMURU HALIMASHAURI ZIKAGUE MAJENGO YALIOYOJENGWA KINYUME NA UTARATIBU YAVUNJWE???? HIVI HII INAINGIA KICHWANI KWELI. YANI HALMASHAURI ZIVUNJE SHERIA ALAFU ZIPITIE TENA ZIJIKAMATE ZENYEWE ZIYYAVUNJE MAJEGO??? MIMI SIJAWAHI SIKIA...LABDA DADA YETU ALIGHAFILIKA.

    IUNDWE TUME HURU KABISA IPITIE HAYO MAJENGO YOTE. HAPO NDIO KUFANYA KAZI MAMA. JANGA LINATUSUBIRI TU TETEMEKO LIKITOKEA.....I HOPE WATAONA SENSE. WANANCHI TUIWAJIBISHE SERIKALI..

    ReplyDelete
  11. Acheni sheria ichukue mkondo wake, wengi hapo msemea hasira, chuki, vivu na njaa. Wahusika wapo na sheria zipo. Ghorofa likianguka waziri ajiurulu, basi likianguka nani ajiuzulu, simba/mamba kila mtu, wanafunzi wakifeli, wagonjwa wakifa, mafuriko yakitokea nk....

    ReplyDelete
  12. wanasema hilo jumba linasemekana limejengwa chini ya kiwango. Kwa hiyo ni hear say tu hapakufanywa utafiti kuthibitisha kuwa hilo jengo limejengwa chini ya kiwango na serikali inatowa amri livunjwe?

    Haya kweli ndio maamuzi ya viongozi wetu? Nawahakikishia wakilivunja hilo mwenye nyumba atafungua kesi na kulipwa mamilioni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...