Wakati hapa kwetu Tanzania aka "Bongo" yaani "Bongo Tambarare" tunalalamikia
kushuka kwa kiwango cha elimu, jirani zetu Kenya au watani wa jadi watoto wao
ndio wana mafanya kweli katika elimu na kuvuna wanachopanda!
mfano hai ni huyu msichana Julie Wang'ombe miaka 22,ndiye aliyezi andika hotuba
za kampeni za Rais Mteule Mhe.Uhuru Kenyatta,na hotuba hizo zikawa ndio dira ya ushindi wa rais huyo.
Hapa kwetu Tanzania tuna kilio na matanga ya kushuka kwa kiwango cha
Elimu ayatakwisha, kama hatua za haraka azitochukuliwa kwa kuipa pumzi za uhai sekta ya elimu, kila siku hitakua tia maji tia maji.
Kuna haja kubwa ya kurudi nyuma na kukaa vikao hili kutafakari wapi ?tulipoteleza
hadi kufikia msiba huu wa Elimu.
Vipi kweli ? nalo hili la kushuka kwa kiwango cha elimu lina hitaji kupiga ramli au kwenda kwa waganga wa jadi kuangilia nani? mchawi wa Elimu yetu.
Nani asiyetetujua watanzania tulivyokua mabingwa wa kuishi kwa Mithali na kugeuza geuza maneno !
Hivi katika kilio hiki cha "ELIMU" nacho tugeuke wasanii wa kugeuza maneno maneno kwa kuukwepa ukweli?
Maana tukiendelea kuutupia kisogo ukweli huu wa kushuka kwa kiwango cha elimu hipo siku tunawakuta watoto wetu wakiwa wapagazi katika ardhi yao wenyewe Tanzania kwa ukosefu wa elimu,na pia tutashindwa hata katika soko la ajira la jumuyia za kiafrika.
KUNA HAJA YA KUJIPANGA NA KUANZA UPYA KAMPENI YA ENZI ZILE ZA KUFUTA UJINGA, ni vema tuanze sasa kujikosoa kuliko kuishi kwa misemo ya jijini Dar ! oh ! One day Yes! lini? Oh ! no sweat ! One day Yes.
Mdau Msema Kweli
SHUKRANI KWAKO MSEMA KWELI, NAKUUNGA MKONO KUWA ELIMU YETU YA SASA NI AIBU KUBWA, LAKINI HATA MIAKA KUMI NYUMA AU ZAIDI ILIKUWA INASHUKA KILA MWAKA LAKINI WAHUSIKA WAKAZIDI KUFUMBIA MACHO NA HAYA NDIO MATOKEO YAKE, TUSIPOBADILIKA TUTAKUWA ZEROOOOOO. LAKINI NA WEWE MSEMA KWELI MBONA KISWAHILI NACHO UNAKOSEA?
ReplyDeleteelimu sio muhimu kwa sababu ya mafisadi wazee wanaoongoza nchi kwa miaka nenda rudi hawataki elimu ipatikane ili vijana waje kuongoza nchi
ReplyDeletewazee mafisadi wanataka kila siku wao ndio wabakie na elimu ili taifa waendelee kuliongoza wao na watoto zao wanaowasomesha shule za gharama
watoto wa walalahoi elimu bora itabaki kuwa ni ndoto sababu hakuna anaetaka wapate hiyo elimu bora badae waje kugombania nafasi za kuongoza nchi na watoto wa mafisadi
tunachokijuwa watanzania ni kuwa ipo siku watanzania walalahoi watakapokuja kuchoka na matokeo yatakuwa mabaya
viongozi tunawategemea leo hii hakuna hata mwenye sauti ya juu kushikilia bango la elimu
kelele zetu ni bure ni sawa na wimbo uliopigwa marufuku wa hayati dr,remmy ongala unaosema
KILIO CHA SAMAKI MACHOZI HUISHIA MAJINI.
kwa kuwabadilisha wabongo ipo kazi kweli kweli,kama waziri na akili zake anasema tuchape viboko watoto ndio watakua na akili,mwenyewe hajui tanzania ni muungano wa nchi gani.Hali inazidi kuwa tete waalimu wamegoma kichinichini eti wamekataa kuwaongeza mshahara.
ReplyDeleteTatizo wakubwa wetu hawathamini vijana tanzania, ukitoka nje wazee huwa wanaamini sana vijana wao na kuwashirikisha katika kila kitu. wazee wetu wakiwa na kijiuwezo basi ndiyo hawataki kabisa mtoto asogee karibu wanasahau kuwa umri unakwenda uzee unakuja na kuwa kama leo alikuwa na uwezo wa kufikiri na kupata idea na kujikimu na maisha miaka 30 ijayo hatakuwa na uwezo kufanya maamuzi kama alivyokuwa miaka 30 iliyopita. mtoto umleavyo ndiyo akuavyo, vijana inabidi wawe trained na hiyo training ianzie nyumbani kwa kushirikishwa katika kila maamuzi, na sio kukalishwa kikao ikiwapo amefanya mabaya kama kunywa pombe au kuiba au kutia mimba mtoto wa jirani.
ReplyDeleteHii Makala ina maneno ya ukweli mtupu isipokuwa kama ilivyojielezea yenyewe pia ina mbwembwe nyingi za Kisiasa ktk jinsi lugha ilivyotumika kuiandika.
ReplyDeleteMchawi wa kushuka kwa kasi ya kutisha kwa kiwango cha Elimu nchini Tanzania sio mwingine bali ni mambo haya hapa chini:
1.TUWE NA UTAMADUNI WA KUKUBALI KUSAHIHISHWA:
Hitilafu ilishaonekana Mhe. Mbunge mmojawapo akatoa Hoja kuhusu udhaifu wa Mitaala ya Elimu ikakataliwa Bungeni, mwezi uliofuata Matokeo ya Mitihadi Kidato cha nne yakawa ni mabaya sana ktk Historia ya Elimu nchini.
2.TUWE NA UTAMADUNI WA KUSHIRIKISHA WATU KTK MASUALA NYETI NA MUHIMU KWA NCHI YETU NA KUJALI MAONI YA WATU NA KUYAFANYIA KAZI: Tuwe na Utamaduni wa kushirikisha watu na kujali Maoni ya watu ktk mambo nyeti.
Mfano unakuta Mikataba mingi na Sera nyingi zinapangwa na kutiwa Saini za Makubaliano na watu wachache na inakuwa ni Siri,
(i)Tumeshuhudia Mikataba mibovu ktk Uwekezaji na tukaona madhara yake.
(ii)Angalieni mambo ya kukurupuka ku saini vitu bila kuwa makini yametuningiza mkenge mfano kusaini uwanachama wa Mahakama ya ICC huku nchi zingine makini kama Rwanda hazijasaini uwanachama huo baada ya kubaini uwanachama wa Mahakama kama hiyo una madhara makubwa baadae, siyo tuchukulie kigezo Maaziomi yote yanayoletwa na Mataifa makubwa mbele yetu ni ya kuyakubali ili tusinyimwe Misaada. mambo mengine tukatae kwa maslahi ya Taifa letu na watu wake.
(iii)Angalieni IMF mwaka 1985 ilitoa Mashariti ya kupunguza wafanyakazi Serilakini Redundance kwa ajili kubana matumizi ya Serikali tukaona madhara yake kwa kuwa Matumizi ya Umma hayatakiwi kudhibitiwa ila yanafuatliliwa kwa makini, angalieni tena IMF hiyo hiyo mwaka 1994 ilituwekea Mahsariti ya kubana matumizi ya Umma kwa kufunga Mafunzo ya JKT na sasa tukaona madhara ya kukosa Mafunzo hayo na kuamua kuyarejesha tena.
3.TUACHE UTARATIBU MBAYA NA HATARI WA KUFIKIA MALENGO KWA NJIA ZA MKATO:
Mfano kufuata utaratibu wa kuwapata Walimu kuwa ni wale wenye Madaraja ya chini ya Ufaulu ktk Mitihani ya Kidato cha 4 na cha 6, kwa kuwa ktk Dunia Elimu ngazi zote kuanzia Chekechea hadi Elimu ya Juu nchi zooote Mwanafunzi aliye faulu zaidi ndiye anayestahili kuwa Mwalimu na sio yule aliyefeli Mtihani wa mwisho.
Mfano Chuo Kikuu anayekuwa Teaching assistant au Mkufunzi Msaidizi huwa anakuwa yule aliyefeli Mtihani?, la anayekuwa Msaidizi Mkufunzi ni lazima awe na alama za juu za ufaulu wa Mtihani.
TANZANIA NI LAZIMA TUFUNGUKE KWA HAYO MATATU (3) HAPO JUU NA TUTIZAME DUNIA INAVYOKWENDA!
Hapa kwetu sasa hivi tuna tatizo la generational change. Wazee wengi wako na vyeo lakini hawaielewi dunia ya leo. Lakini pia hawataki kupumzika. Wazee watoe nafasi kwa vijana. Huyu Naibu Waziri si mzee, ila ufahamu wake ni mdogo sana haufai. Nchi zenye elimu bora kama Canada, Sweden na Finland hawachapi viboko mbona wana elimu bora?!
ReplyDeleteMtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Walezi jitazameni kabla ya kuonesha vidole wengine.
ReplyDeleteHayo makosa aliyoyataja sasha eve ni makubwa mno, kunywa pombe, kuiba, uzinifu nk.. mwisho atasema uuaji nao ni kosa dogo.
ReplyDeleteLakini katika swala la elimu,ni kweli kabisa kama alivyododosa msema kweli,kuwa tunaishi kwa kupiga ramli na kutafuta nani mchawi wa kifo cha elimu,sidhani kuwa ni busara kuanza kwenda kwa waganga wa jadi kumtafuta mchawi wakati ukweli tunaujua,kuwa elimu kwetu ni sawa na kituo cha polisi.
ReplyDeleteTunamsubiri mungu ashushe malaika kutoka mbinguni wajekuleta uokovu katika msiba huu wa kifo cha elimu.
ReplyDeletekwa jina la baba,na la mwana,na la
Roho mtakatifu,
Mungu walete malaika waje kutuokoa
Amin
Kazi kweli hivi tunategemea nini? wakati sisi wazazi tunapigania mashuleni lazima kuwepo somo la bongo fleva,
ReplyDeleteNjia za makato katika kusaka elimu kwa kuanzisha shule zisizo na viwango vya ubora wa walimu kumeifanya sekta ya elimu kuwa mtaji wa biashara ya mafisadi
Jamani, tuache kukosoa kwa kulinganisha tu, mimi ningeridhika kama muandikaji/mchangiaji akisema ufumbuzu ndio huu!Matatizo na changamoto tunazujia na tumekua tukiongelea kwa miakaaa yote toka miaka 10 ya uhuru 1971. TZ inahitaji waliowengi KUELIMIKA maana waliosoma sasa ni KIBAO na miaka yote wanaongezeka. TOA Ufumbuzi kwa jinsi unavyoona.
ReplyDeleteKAMA KAWAIDA TULIKUWA TUMEPOTEZEA ILI MSAHAU SASA NAONA MDAU UNAKUMBUSHIA TENA ILE ISSUE YA 60%. SUBJECT YAKO HAPA ILIKUWA HUYO BINTI ALIYEANDIKA HOTUBA YA RAIS NILITARAJIA UNGETUPA DETAILS ZA HIYO HUTUBA LAKINI KUMBE OBJECTIVE YAKO ILIKUWA KULENGA PALE PALE TULIPOKUWA TUMEPAPOTEZEA. NINA MASIKITIKO KWA VILE NAMI JAMAA ZANGUA WAMEDUMBUKIA KWENYE HII BOAT YA MV 60%. ANYWAY, BIG UP SANA KWA JULIE NA KWA UMRI WAKE SIDHANI KAMA KUNA CHA KUSHANGAZA KWANI YUKO KATIKA LEVEL YA UNIVERSITY SIDHANI HILO LITATUSHINDA HATA SISI WATANZANIA WA UMRI KAMA WAKE
ReplyDeleteNi ajabu na kweli!
ReplyDeleteKama Mwingereza alitutawala tukapata Uhuru mwaka 1961 tukaanza kuendesha mambo yetu wenyewe, nadhani Suala la Elimu tumkabidhi tena Mwingereza (Mkoloni wetu) kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania atoe Elimu nchini sisi tubaki na mambo mengine ktk nchi.
Msichana Lilian Mwang'ombe umri miaka 22 wa Kenya huyo ni kuwa yupo ktk ngazi ya Elimu ya Sekondari tu, yaani wenye umri wa miaka 18-22 ndio wanasoma ama wamemaliza Elimu ya Sekondari.
Sasa kwa hapa Bongo/TANZANIA unaweza kukuta mtu amemaliza Chuo Kikuu (Graduate) Umri zaidi ya hiyo miaka 22 ya Msichana wa Kenya lakini hata Barua ya kuomba Kazi hajui kuandika, Barua ya Biashara hajui, Kiingereza chake brocken, hajui pia kujieleza kwa Kiingereza Fasaha!
Mmeona Kiama cha kuanguka kiwango cha Elimu nchini hapo?