Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi ya Umeme, Gesi, Bajeti ya Serikali pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi ya gesi. Mkataba huo umesainiwa leo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa Waziri wa fedha, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier Mjini Washington DC.

Waziri wa Fedha Mhe Dkt. Wiliam Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakati wa kusaini mikataba hiyo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi. Susan Mkapa pamoja na wanasheria wa Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini wakati Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakitia sahii mikataba hiyo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa wakibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier. Picha na mdau Ingiahedi mduma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...