Moja ya timu zijazotumia uwanja wa Majimaji ikijitupa uwanjani kusukuma gozi. Uwanja umeharibika pitch, sehemu za kukaa, vyoo nk. Unahitaji ukarabati mkubwa. Shukrani kwa Hayati Dr Lawrence Gama kwa kujenga uwanja huu. Alikua bado hajaukamilisha.
Wachezaji wa timu ya Majimaji Kabla ya kupiga mechi ya mwisho ya ligi daraja la kwanza. Hata hivyo wameshindwa kufuzu kucheza ligi kuu msimu ujao Baada ya kuzidiwa point na Mbeya City waliopanda daraja. Majimaji ilikua mshindi wa pili na hivyo Wananchi wa Songea na Ruvuma wataendelea kuisikia ligi kwenye radio na kuitazama kunako TV
eneo la Hightable uwanja wa Majimaji.Picha na Mdau Gerson Msigwa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wamwite Kibadeni na John Kabisama waushughulikie huo uwanja. Hao ndio wakongwe wa hiyo Timu.

    ReplyDelete
  2. Very sad indeed! Wakati nasoma na kucheza mpira Songea Boys, aka Box II, kule Luhira, uwanja huu ulikuwa among the best kusini yote!

    I have memories of playing here and scoring goals enzi za UMISETA!! Tulimaliza hapa na tuliochaguliwa timu ya mkoa tukaenda kucheza Umoja stadium ya Mtwara, wakati ule lilikuwepo jukwaa moja tuu, sijui siku hizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...