Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (kushoto) akiwa chini ya ulinzi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam pamoja na watuhumiwa wenzake kumi.
Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (kulia) na watuhumiwa wenzake kumi wakisubiri kupandishwa kizimbani, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (aliyevaa kanzu nyuma) akiwa na watuhumiwa wenzake mara baada ya kupandishwa kizimbani na watuhumiwa wenzake kumi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Picha na Francis Dande
Mfanyabiashara Radha Hussein Ladha wa jijini Dar es Salaam, Diwani katika Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki (59) na wenzao 9, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 24 ya kuua bila ya kukusudia.
Katika kundi hilo pia wamo wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala ambao ni Mhandisi Mkuu, Mhandisi Charles Salu (48), Mhandisi wa Majengo Godluck Sylivester (35) Mbaga na Mkurugenzi Mkuu wa Mkaguzi wa Majengo, Willibrod Wilbard (42).
Washtakiwa wengine ni Mhandisi Mohamed Swaburi (61), Mhandisi Mshauri, Zonazea Oushoudada (60), Mkadiriaji Majenzi, Vedasto Nziko (59), Msanifu Majengo, Michael Hema (59), Msajili Msaidizi AQRB, Albert Mnuo na Ofisa Mkuu Mtekelezaji OQRB, Joseph Ringo.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka, Wakili wa Serikali, Tumain Kweka akisaidiana na mawakili wenzake watano, alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa kinyume na kifungu cha 195 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Kweka anasadiana na wenzake Benard Kongora, Ladslaus Komanya, Neema Haule, Joseph Maugo na Mutalemwa Kishenyi.Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja Machi 29, mwaka huu katika Mtaa wa Indira Gandhi, Wilaya ya Ilala waliwaua bila ya kukusudia Yusuph Mohamed, Kulwa Khalfan na Hamada Mussa.
Mbali na watu hao, pia wanadaiwa kuwaua bila ya kukusudia Kessy Manjapa, Khamis Mkomwa, Boniface Benard, Suhail Ally, Salmani Akbar, Seleman Haji, Seleman Mtego, Sikudhani Mohamed, Ahmed Milambo, Salum Mapunda, Suleiman Rashid na John Majewa.
Wengine ni Mussa Mnyamani, David Severin Herman, William Joackim, Abdulrahman Mwiha, Emmanuel Christian, Mmanyi Ngadula, Adivai Desiki, Emmanuel Greyson na Augustino Kasiri.
Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mashtaka yanayowakabili Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza hadi Mahakama Kuu.
Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mashtaka yanayowakabili Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza hadi Mahakama Kuu.
Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili wa Kujitegemea, Jerome Msemwa waliiomba mahakama kutoa dhamana kwa wateja wao kwa sababu mashtaka ya kuua bila ya kukusudia yanayowakabili yanadhaminika.
Wakili wa Serikali, Kongora alipinga maombi hayo, huku wakili mwenzake Komanya akisema kuwa wakati huu si wa kutoa dhamana kwa kuzingatia mazingira ya tukio lililosababisha kuwepo kwa kesi hiyo.
Kutokana na hoja hizo, Hakimu Kisoka aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 16, mwaka huu atakapotoa uamuzi iwapo washtakiwa wapate dhamana ama la.
Haya ni mashitaka ya kukusudia! Haiwezekani wajenge kwa kiwango kisichotakiwa then tuseme hawakukusudia!
ReplyDeleteMdau, kwa bahati mbaya tafsiri ya "kukusudia kuua" kisheria inaangalia mambo mengi. Nadhani unakumbuka jinsi kesi maarufu ya askari waliouwa wafanya biashara wa madini walivyoshinda kirahisi na watu wengi wakalalamika, kwa kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha kuua. Kama wangeshitakiwa kama kesi hii nadhani maamuzi yangekuwa tofauti. Tatizo langu kubwa ni kuwa kuna maghorofa mengi ya namna ile ile na yanatumika hasa kariakoo na katikati ya jiji kwa hiyo tujitayarishe kwa maafa makubwa!!
ReplyDeletehaya ndugu zanguni matokeo ya rushwa ni mabaya sana na huu ndio mwisho wake. Nakumbuka nikiwa dar nilijaribu sana kupata kibali halali cha ujenzi wa kanyumba kangu lakini kila nikienda manispaa nilizungushwa mpaka nikakoma. Mwisho wa siku nikaambiwa ili kibali kitoke nitoe kitu kidogo wakati ni haki yangu na nyumba yenyewe ni ya chini (si ghorofa).
ReplyDeleteAnyway nilishindwa nikaacha na wengine wakaniambia nijenge tu bila kibali maana wengi wanajenga bila kibali kwa sababu ya rushwa nzito iliyojaa kwenye kutoa vibali. Mshahara wa rushwa mwisho wake mbaya sana maana kama huridhiki na mshahara ni bora kuacha kazi na labda kufanya biashara kuliko kuchukua rushwa inayokuja kuua watu.
mdau
uswis
Ghorofa kujenga katika Bongo Tambarale kila mmoja anaweza !
ReplyDeleteBongo kila kitu kinawezekana, Tajiri anatumia Shilingi Milioni 800 kujenga Ghorofa na mimi BANDEKO ZOMBOKO kwangu Vungunguti natumia Shs. 200,000/= (Laki mbili) kujenga Ghorofa!!!
Mnabisha?
Mbona babu yangu kule Undengerekoni amejenga Dungu tena shambani akitumia kulindia mpunga usiliwe na ndege?, ile pia si Ghorofa au mtakaa?
Ujenzi wa kitu chochote kiendacho angani liwe Gorofa ama Dungu la kulindia Mpunga shambani Kanuni zake ni zile zile kama Jengo lililoanguka wiki iliyopita!
Sasa kulikuwa kuna ajabu gani babu yetu Mzee Raza Hussein Ladha kutumia Shs. 200,000/= (LAKI MBILI TU) Badala ya Shs. 2 Bilioni kujengea Ghorofa la sakafu 16 kwenda juu?
Loooh,
ReplyDeletehao jamaa wengine 10 watakuwa wameponzwa na Rushwa za Shs. 10,000/= kila mmoja,
masikini weee Babu amewasainisha wakampitishia aendelee na mradi wake wa ujenzi na sasa wanamezwa na mamba!
Weee babu muogope Mwenyezi,
ReplyDeleteAcha kumchezea Mwenyezi Mungu!
Wakati unahujumu hukuwa na Mwenyezi, sasa baada ya mauaji huku ukiwa unaburuzwa Mahakamani unamgeukia Mwenyezi na ndio unakumbuka kubeba Tasubihi mkononi?
Kuua bila kukusudia?
ReplyDeleteEbooo haya Mashitaka yaandikishwe upya msitutie hasira hapa!
Yaani kwa kiwango kile cha ushenzi na kukosa ubinaadamu hadi kupelekea mauaji waliyosababisha vifo kwa watu wanyonge wasio na hatia halafu mnasema wameuwa bila kukusudia!
Sasa mlitaka wauwe vipi ndio mseme wamekusudia?
Mlitaka labda eneo lote la Mtaa au ule Msikiti mzima nyuma ya eneo la maafa ungeangukiwa na wooote wafe ndani siyo ndio mngesema wamekusudia?
Uzembe wao katika kazi na Ufisadi wa baadhi ya wadau ndiyo makusudio yao ya Kuua bila kujali
ReplyDeleteInasikitisha sana miaka hii ya 2013 vitu kama hivi kutokea, tulioko huku nje kila siku tunasikia bongo tambarale, maghorofa yanazidi kujemgwa ujenzi wenyewe mbovu watu hawafuati sheria matokeo yake wanaua watu. Wahusika please angalieni hili swala kwa makini ili kuokoa maiosha ya watu, watu 36 ni wengi mno kupoteza maisha katika mazingira hayo, feel for those who lost their loved ones... it could have been you! my heart goes out to you all. Toronto
ReplyDelete